SHIRIKISHO la Riadha la Taifa (RT) limezitangaza rasmi mbio za Rock City Marathon kuwa mbio za kimataifa baada ya kukidhi vigezo vyote ikiwa ni pamoja na kuhusisha mbio za km 42 kwa mara ya kwanza. Hatua ambayo imepongezwa na wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, na Kagera kwa kuwa itachochea ukuaji wa utalii katika kanda hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha mbali na kupongeza hatua hiyo alisema uwepo wa mbio hizo katika kalenda ya Riadha kimataifa itawavutia watalii wengi katika ukanda huo pia na hivyo kufungua fursa zaidi kupitia utalii.
“Tunatarajia kwamba sasa mbio hizi zitafahamika zaidi duniani na kuvutia washiriki wa kimataifa ambao tunatarajia pia watakuja kama watalii na pia watapata kufahamu fursa za kiuwekezaji,’’ alisema.
Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack alisema Mkoa wake unaenda kujipanga kuhakikisha kwamba unatoa washiri bora katika mbio hizo huku akitoa wito kwa waandaaji wa mbio hizo kwa kushirikiana na viongozi wa riadha nchini kuhakikisha wanazitangaza kimataifa mbio hizo ili zivutie washiriki wengi wa kimataifa watakaokuja na fursa nyingine za kiuchumi ikiwemo sekta ya utalii na uwekezaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama alisema Mkuu wa Wilaya ya Butiama,Bi Annarose Nyamubi aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa alisema mkoa wake unatarajia kunufaika na mbio hizo kimataifa kupitia vivutio vya kitalii vilivyopo kwenye mkoa huo ikiwemo utamuduni wa wakazi wake pamoja na kuwavutia watalii kutembelea kaburi na kumbukumbu nyingine za Hayati Mwl Julius Nyerere.
Mbio hizo zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA, Mwanza Hotel , Real PR Solutions Limited, Fabec na Afrimax Strategic Partnerships Limited.
Awali akitangaza mbio hizo kuwa kimataifa, Makamu wa pili wa RT, Dk Hamad Ndee alisema hatua hiyo inatokana na mbio hizo kukidhi vigezo vyote muhimu ikiwemo upimaji wa njia za kukimbia uliofanywa kitalaamu na mpimajia anayetambuliwa kimataifa Bw John Bayo pamoja na kuhusisha kwa mara ya kwanza mbio za KM 42.195
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi mbali na kujipongeza kwa hatua hiyo alisema uhusishaji wa wawashiriki wengi wa kimataifa katika mbio hizo utakidhi lengo hasa la kutangaza utalii katika ukanda wa Ziwa ambayo ni moja ya agenda kuu ya mbio hizo ukiondoa ile ya kuibua na kukuza vipaji vya mchezo huo.
“Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo lazima vitangazwe kimataifa kwa nguvu kubwa na zaidi ni rahisi kwa watalii kufika hifadhi kama ya Serengeti akitokea Mwanza kuliko kanda nyingine,’’ alibainisha.
Alisema mwaka huu mbio hizo zimezinduliwa mapema ili kutoa muda wa kutosha kwa washiriki waweze kujiandaa vizuri zaidi ili waweze kutoa ushindani zaidi huku akitaja makundi mengine ya mbio hizo kuwa ni kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2.5 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 10.
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Rock City marathon mwaka 2017 wakati wa hafla fupi ya
uzinduzi huo iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia
ni pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi (kulia) aliemuwakilisha mkuu
wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi (wa pili kushoto) na Makamu wa pili wa
Shirikisho la Riadha Taifa (RT), Dk Hamad Ndee. Bi Tesha alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack akitoa nasaa zake kwenye hafla
fupi ya uzinduzi wa Rock City Marathon uliofanyika jijini Mwanza
mwishoni mwa wiki. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa
ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu
katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza kwa uratibu wa kampuni ya
Capital Plus International.
Mpimaji
wa njia wa njia za riadha anayetambulika kimataifa Bw John Bayo
akimuonyesha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa njia zitakazotumika
katika mbio hizo baada ya kupimwa kitaalamu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Makamu wa pili wa RT, Dk Hamad Ndee akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Butiama,Bi Annarose Nyamubi aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa
wa Mara Dk. Charles Mlingwa akizungumza kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.
Meneja
Mkuu wa Hotel ya New Mwanza Hotel Bw Senthi Kumar akizungumza kwenye
uzinduzi huo kwa niaba ya wadhamini wengine wa mbio hizo. Hotel hiyo ni
moja ya wadhamini wa mbio za Rock City Marathon.
Wageni wote wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mchezo wa Riadha pamoja na waandaaji wa mbio hizo.-
No comments:
Post a Comment