Sekta
ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia
zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka
huu wa fedha.
Hayo yalisemwa Jana na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi
wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni
ya Taifa (TBC1).
“Utalii unatoa mchango
mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba
unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya
kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na
kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa
maendeleo ya watanzania wote.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjNMLhLGe8ojCM4VXGAaom-AgpAz34Njy-H7PIAAl8ufY6EtB74JM4jMGQlzdsIHv61KjAhnAQfleoaATCunCKcGMCQlbMwKL9ykIzYox1bLHQ3NUc6Y-nv6NVapuLtqZ7WwQLeJXEmtXs/s320/lake-chala3.jpg)
Aliongeza kuwa Tanzania
ina vivutio vingi kama vile Mito, Mabonde, Milima, lakini hifadhi za Taifa kama
Vile Ngorongoro, Serengeti, Gombe, Ruaha ndizo zinazoongoza kwa kuchangia pato
la taifa kwa zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na vivutio vingine.
Bwana Kijazi aliongeza
kwa kusema kuwa, utalii nchini umekuwa ukikuunaongezeka kila mwaka ambapo kwa
takimwu walizo nazo zinaonesha kuwa, ongezeko la watalii kwa miaka mitano iliyopita
limekuwa lilkiongezeka kwa asilimia 4 hadi 7 kila mwaka.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0FNYzXkXUpykeazOkYtdbvIbNn_brAkAHT76XPQiV3ShDxzyqdkXcv1bht50Z8JyxFjlHAanA9ftu-LO-3NwGBDxXDsg4ecTmXXweK0R0M-JaS_rz0esEL9CsDglBxzWdtX1cLT8fllM/s320/static1.squarespace.com.jpg)
Mkurugenzi Kijazi
alisema kuwa, Mataifa yanayoongoza kutembelea hifadhi za taifa ni pamoja na
Marekani, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, pamoja na Hispania huku akitaja
kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Nchini hasa hifadhi ni vya kipekee, mazingira mazuri,
hali ya hewa pamoja na amani na utulivu uliopo nchini ndiyo sababu zinazowavutia watalii kuongezeka kila mwaka.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMt90pQT6HsRE0M5Aj_9p8yYyv4wJS5Wh2xwVbIUA1HmBayIde-mKCTdF6jIYYqbI477lzk8dBXy9qU82H1oX1cEGLvL4V9NYnOAZe5Rku3aevkllKsvQ7jwXn9RJk8TYImWcFyDGgaeA/s320/zanzibar-91_high.jpg)
Hivi karibuni Mtandao
wa SafariBookings.com unaojihusisha na masuala ya ukuzaji wa safari za kitalii
barani Afrika uliitaja Tanzania kama kivutio kizuri cha safari za
watalii barani humu.
No comments:
Post a Comment