Sunday, July 9, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Watu sita wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na jeshi la polisi wakati walipokuwa wakijaribu kutoroka katika maficho yao mkoani Mwanza. https://youtu.be/WfxqZqglz48

SIMU.TV: Taaisi ya Aghakhan inatarajia kujenga chuo kikuu cha Agakhan, taasisi ya moyo na saratani ili kupunguza gharama za wananchi kwenda kutibiwa nje ya nchi. https://youtu.be/xy6uM89q9JA

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Mhuga ametoa agizo la siku saba kwa watu wote waliovamia misitu ya TFS kuhama mara moja. https://youtu.be/HJaqCmOfv9I

SIMU.TV: Jamii imeshauriwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi. https://youtu.be/WZ4gI1e0bR4

SIMU.TV: Serikali imeipongeza timu ya taifa Taifa stars kwa kuipeperusha vyema bendera ya taifa kwenye mashindano ya COSAFA yaliyo fanyika nchini Afrika Kusini. https://youtu.be/6L5n9C-OdIQ  

SIMU.TV: Serikali imesema inajipanga kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta ya sanaa ili nao waweze kuwaajiri wengine. https://youtu.be/n8pPPB-rBXw
SIMU.TV: Mchezaji nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya Houston Rockets James Harden amesaini mkataba wa kuendela kuichezea timu hiyo hadi mwaka 2023. https://youtu.be/SlRl09kDjNs

SIMU.TV: Mwanamuziki na mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama Profesa J jana ameuaga ukapera kwa kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu. https://youtu.be/J8omKyyK4cA  

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwauwa majambazi sita kati ya nane waliokuwa wamejificha wakipanga mikakati ya kufanya uhalifu. https://youtu.be/2W-UAuVy8vY
SIMU.TV: Ongezeko la watu lisilo endana na upatikanaji wa huduma za jamii kama vile kwenye sekta za afya maji na upatikanaji wa ajira ni moja ya changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea. https://youtu.be/Qy7FSlHv68A

SIMU.TV: Halmashauri za mkoa wa Iringa zimeingiwa na wasiwasi kuwa wafanyabiashara wakubwa watasafirisha mazao kwa kutumia magari madogo ili kukwepa ushuru. https://youtu.be/a6fFtye6ArM

SIMU.TV: Wananchi wa kijiji cha Katambike katika halmashauri ya Nsimbo wameiomba serikali kuwajengea zahanati na shule mbadala baada ya zilizopo kutakiwa kubombolewa kutokana na kujengwa kwenye hifadhi ya Reli. https://youtu.be/1TkE0Ztzht8

SIMU.TV: Jamii nchini imeshauriwa kuwatembelea wafungwa na kuwafariji kwa misaada ya kibinadamu kwa maana serikali haiwezi kuwatimizia mahitaji yote. https://youtu.be/Vh2y9jZzm3c

SIMU.TV: Balozi wa klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini England amewasili nchini ikiwa ni siku chache kabla ya klabu hiyo kuja hapa  nchini kucheza na timu ya Gormahia ya nchini Kenya. https://youtu.be/ldsvsWhWWvM

SIMU.TV: Chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam kimetoa tathimi kuelekea kumalizika kwa ligi ya mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam. https://youtu.be/9Wqay4OQ1HE

No comments: