Thursday, July 13, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI imeeleza kuokoa zaidi ya milioni 300 kufuatia kufanya uaosuaji wa moyo kwa wagonjwa 20 hapa nchini. https://youtu.be/4PQ97DBnamE

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akemea tabia za wakuu wa shule mkoani humo kuruhusu shughuli za kisiasa katika shule zao. https://youtu.be/E_BcNXoMVsM

Mamlaka ya mapato nchini TRA yafungia baadhi ya vituo mafuta jijini Dar es salaam kwa kosa la kutotoa risiti za kieletronic na kukosesha serikali mapato. https://youtu.be/EZCHJ-G8ucY

Maonyesho ya 41 ya kibishara ya kimataifa maarufu kama sabasaba, yafungwa rasmi huku wito ukitolewa kwa TANTRADE kushirikisha wadau mbalimbali ili kufanya maboresho. https://youtu.be/TzmGj3bnUIo

Wakazi wa mkoa wa Tanga waanza kunufaika na ujenzi wa Bomba la mafuta toka Uganda, kufuatia baadhi ya wananchi kujipatia ajira. https://youtu.be/U_VPtg7PNds

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof.Makame Mbarawa watiliana saini makataba na waziri wa uchukuzi wa Uganda kushirikiana kuboresha miundombinu ya Bandari, reli, na usafiri wa majini kuanzia Dar es salaam hadi Uganda kupitia Mwanza. https://youtu.be/AsT8jNTfkAw

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali leo imehairisha mahojiano na Mh.Lowassa hadi ifikapo Alhamis wiki ijayo. https://youtu.be/R6Wpjjwn-9Q

Zaidi ya abiria 400 jijini Mwanza wamekwama kusafiri baada ya SUMATRA  kuzuia meli ya Mv Nyehunge isiendelee kutoa huduma za usafiri kuelekea kisiwa cha Ukerewe. https://youtu.be/3nWoma034Do

Ujenzi wa daraja la Tuangoma katika eneo la Kijichi jijini Dar es Salaam umeendelea baada ya kutatuliwa kwa vikwazo vya fidia kwa wananchi. https://youtu.be/k1i5sjVwqRI

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amepokea walimu 18 wa kujitolea kutoka nchini Marekani kwa ajili ya kufundisha shule za msingi sekondari na vyuo vikuu jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/WOD0R6AegPk

Wasindikaji wa vyakula vya nafaka hapa nchini wametakiwa kuzingatia njia salama za usindikaji ili kuwaepusha walaji na madhara ya sumu kuvu ya kuhifadhia nafaka. https://youtu.be/69XAz04igi8

Kufukiwa nyayo za Zamadam katika eneo la Laitoli lilopo kwenye hifadhi ya Ngorongoro imesemekana kupunguza idadi ya watalii waliokuwa wakitembelea eneo hilo. https://youtu.be/y7425N0W9sc

Uhamasishaji wa uchangiaji wa damu salama katika taasisi mbalimbali hapa nchi kumesaidia kuongezeka kwa akiba ya damu tofauti na hapo awali. https://youtu.be/sGA5M_UKJNQ

Serikali imezitaka taasisi za kifedha zinazotoa mikopo midogo midogo kwa wajasiriamali kutoa kwanza elimu juu ya mikopo kwa wajasiriamali wanaotaka mikopo hiyo. https://youtu.be/fQZWL36-uLg

Bodi ya utalii nchini TTB kwa kushirikiana na shirika la reli Tanzania na Zambia TAZARA wameamua kutumia usafiri wa reli katika kukuza utalii kwa nchi hizo mbili. https://youtu.be/n0Yzw00lmpI

Serikali imeziasa taasisi za umma zinazoshughulikia viwango vya bidhaa nchini kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza urasimu. https://youtu.be/oWVkZaAt9bs

Wachezaji wa gofu wa klabu ya gofu ya Lugalo wameondoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro kushiriki mashindano ya wazi ya gofu yatakayofanyika mkoani humo. https://youtu.be/IfrM4fqqXVo

Jumla ya wachezaji sita wa riadha na kuogelea wamekabidhiwa bendera ya taifa tayari kuelekea nchini Bahamas kushiriki michuano ya jumuiya ya madola. https://youtu.be/wz1lag-uzs4

Bondia Floyd Maiwether na mpinzani wake McGregor wameendelea kutupiana maneno ya kejeli kuelekea pambano lao litakalofanyika mwezi August. https://youtu.be/JdBY-CklHs4

Timu ya Everton inayochezea ligi kuu nchini Uingereza imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/pv_gCWPjQlc

Kamati ya Olympic Tanzania imekabidhi bendera ya taifa kwa timu za riadha na kuogelea zinazoenda kushiriki mashindano ya jumuiya ya Madola huko nchini Bahamas. https://youtu.be/rGVWS5UFLuw

Kesi inayowakabili viongozi wa klabu ya Simba Evance Aveva na Nyange Kaburu imeairishwa hadi julai 20 mwaka huu na watuhumiwa wamerudishwa rumande. https://youtu.be/R800FAHK6Ws

No comments: