Wednesday, July 5, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli tayari ametia saini miswada miwili ambayo iliyojadiliwa na kupitishwa na bunge. https://youtu.be/FnZQyp0gf8A

SIMU.TV: Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo amearisha bunge hadi tarehe tano mwezi wa tisa. https://youtu.be/dDaa6qeGKWI

SIMU.TV: Katibu mkuu wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amevitaka vyombo vya habari kushiriki katika kuelezea dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. https://youtu.be/cqx_bk9gK2M

SIMU.TV: Chama cha kuweka na kukopa cha walimu wa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu chenye mtaji wa shilingi bilioni mia mbili kimeshauriwa kuwapa wanachama wake mikopo yenye riba nafuu ili kiweze kukuza mtaji wake. https://youtu.be/SyuwN3S3NJ4

SIMU.TV: Serikali imewataka watoa huduma za afya nchini kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu ili waweze kupatiwa huduma za matibabu na kutokomeza ugonjwa huo. https://youtu.be/mlPv8BHKch4

SIMU.TV: Watu wenye ulemavu mkoani Arusha wamehimizwa kutumia fursa zilizopo kujiendeleza kiuchumi ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha https://youtu.be/9OyHEnKh_tw
SIMU.TV: Waziri wa Tanzania Kassim Majaliwa amewahakikishia watanzania kuwa nchi iko salama na serikali itaendelea kuitunza amani iliyopo; https://youtu.be/HQZzQE3O0rs

SIMU.TV: Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka viongozi wa ngazi za kata kuunda vikundi vya ulinzi kusaidia jeshi la polisi kuimarisha ulinzi na usalama; https://youtu.be/Se-fBCASuIk

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu amerejea nchini akitokea nchini Ethiopia ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika; https://youtu.be/LM6c3DWiv1I

SIMU.TV: Soko kuu la manispaa ya Kigoma Ujiji linakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo uhaba wa choo, maji pamoja na uchakavu wa miundombinu; https://youtu.be/_2r_RtmZT8E

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imesema kuwa inaendelea kufuatilia kwa ukaribu taarifa za madereva 18 wa kitanzania waliotekwa na waasi nchini Congo DRC; https://youtu.be/1eRlpAhkABw

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyakazi katika mgodi wa Buzwagi mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro baina yao na wamiliki wa mgodi huo; https://youtu.be/aM2oevgbMuA

SIMU.TV: Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Amour ameishauri halmashauri ya Itilima mkoani Simiyu kuunda jumuiya za watu wanaotumia maji; https://youtu.be/C10Idx70bZk

SIMU.TV: Serikali imepokea gawio la shilingi bilioni 10 kutoka katika kampuni ya Puma Energy, Kampuni ya Tipa na TBP Bank baada ya taasisi hizo kujiendesha kwa faida; https://youtu.be/248sFcKB028

SIMU.TV: Bodi ya maziwa Tanzania imewataka wauzaji wadogo wadogo wa maziwa kujiunga katika vikundi ili waweze kufanya biashara kwa urahisi; https://youtu.be/pDFCpMJSw10

SIMU.TV: Benki ya Covenant inahamasisha  wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania kujiunga katika bima ya matibabu katika hospitali za AAR; https://youtu.be/spVefiAneZ4  

SIMU.TV: Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imeaga mashindano ya Cosafa baada ya kukubali kichapo kutoka kwa timu ya Zambia Chipolopolo cha mabao 4-2; https://youtu.be/GSphKdT7t2Q

SIMU.TV: Serikali imesema kuwa haitawavumilia hata kidogo baadhi ya viongozi ambao watajaribu kukwamisha juhudi za kukuza soka la Tanzania; https://youtu.be/oDijpRGDygI

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji wao mpya Ibrahim Ajib ambae amesaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria; https://youtu.be/klsqvkD1fIw

SIMU.TV: Shirika la utangazaji nchini TBC limepanga kukuletea makala maalumu endelevu kuhusiana na mchezo wa ngumi za kulipwa; https://youtu.be/Faqc7hYzA5w

No comments: