Thursday, July 27, 2017
SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa akizungumza leo katika warsha ya siku tatu jijini Arusha iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini , mafunzo hayo yanalengo lakuwajengea uwezo watetezi hao ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha).
Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu,THRDC Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri watetezi hao wakajengewa uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya Nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji.
Katibu mkuu chama cha wafugaji Tanzania Maghembe Makoye alisema kuwa Tanzania inamifugo na wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili kuhakikisha kundi hilo haligombani
Makamu Mwenyekiti Taifa Esther Laban Alimuomba Rais Magufuli kuangalia namna ya kuwaelimisha zaidi Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Arusha kwa semina ya siku tatu
Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali imewaomba viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania pamojana watetezi wahaki za wafugaji kuhakikisha wanaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara Nchini hali ambayo imekuwa ikirUdisha maendeleo nyuma
Akizungumza jijini hapa katika ufunguzi wa warsha ya siku tatu iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini ,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa alisema kuwa lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo hao watetezi ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii
“Serikali tunaomba sana watetetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na wahamasishe uwanzishwaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Raisi Magufuli katika sera ya viwanda”Alisema Mwakiposa
Aidha alisema kuwa sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri watanzania walio wengi zaidia asilimia 70 na ndio sekta pekee ambayo haiitaji elimu kubwa tofauti na ajira za viwandani na sehemu nyingine hivyo ni muhimu kujengwa uwezo ili kutimiza sera ya viwanda hapa nchini
Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu,THRDC Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri wakajengewa uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya Nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji
“Tunaamini kuwa watetezi hawa wakifahamu vizu sera na sheria wataweza kuangalia mifumo ya utoaji haki kama haitendeki kwa wafugaji wataweza kutumia fursa hiyo kuwatetea vizuri”
Katibu mkuu chama cha wafugaji Tanzania Maghembe Makoye alisema kuwa Tanzania inamifugo na wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili kuhakikisha kundi hilo haligombani
“Nivizuri tukihamasishana kufuga kisasa ili kujiongezea tija katika uzalishaji wa bidhaa za wafugaji sanjari na kupata masoko ndani na nje ya nchi “
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment