Wednesday, July 19, 2017

SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kwiyeko alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi wa umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw, Msongela Palela akiwasilisha taarifa ya manispaa anayoiongoza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alipofanya ziara ya kikazi  katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule – Manispaa ya Ilala, Bi. Juliana Mhonyiwa akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa.

“Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana na mpango.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu mbalimbali.

Aidha, Mhe. Kairuki amesema kwa sababu ya kutoshirikishwa wapo wanaopotosha kuwa Serikali imefuta Mpango wa Mafunzo. “Napenda kuwaambia kuwa Serikali haijafuta mafunzo, ili mtumishi wa umma aweze kufanya kazi zake kwa weledi ni lazima ahudhurie mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kusisitiza Serikali inajali mafunzo kwa rasilimaliwatu kwa matokeo bora.

Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni siku ya nane akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

No comments: