Friday, July 28, 2017

NAIBU WAZIRI UTALII NA MALIASILI INJINIA RAMO MAKANI AFUNGA RASMI MKUTANO WA SITA WA TANAPA KWA WAHARIRI NA WAANDISHI WAANDAMIZI MKOANI TANGA



Naibu Waziri Maliasili na Utalii Injinia Ramo Makani leo akizungumza jambo wakati akifunga rasmi Mkutano wa Mwaka na Wahariri na Wanahabari Waandamizi nchini jijini Tanga.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Injinia  Ramo Makani akimkabidhi
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda cheti cha ushiriki wa Mkutano wa Mwaka na Wahariri na Wanahabari Waandamizi nchini uliohitimishwa jioni ya leo jijini Tanga.Katika hatua hiyo ya kukabidhiwa vyeti,washiriki wote walikabidhiwa vyeti vya ushiriki wao kwa ukamilifu katika mkutano huo.

Mgeni rasmi,Naibu Waziri Maliasili na Utalii Injinia  Ramo Makani(wanne kulia) akiwa katika picha ya pmoja na washiriki wa Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.

Sehemu ya Meza kuu,kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF),Theophil Makunga,Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Dkt.Hassan Abbas,Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa ,Mgeni rasmi-Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani,Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mhe.Thobis Mwilapwa.

Baadhii ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo kabla ya kufungwa rasmi jioni ya leo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akiwashukuru washiriki wa Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,na kuhitimishwa rasmi jioni ya leo na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani .
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh.Thobias Mwilapa akizungumza niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh.Martin Shigella wakati wa kutoa salamu za shukurani kabla ya kufungwa rasmi kwa Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.

 Meneja Mahusiano wa TANAPA,Pascal Shelutete akizungumza jambo kabla ya mgeni rasmi kufunga Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga.

No comments: