Saturday, July 8, 2017

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) PROF. MOHAMED JANABI ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza viongozi mbalimbali waliotembelea viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi Taasisi yake inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya Moyo na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi wakati alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. 


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aika Nnkya akimsikiliza Haubert Makoke ambaye alimuuliza swali kuhusu magonjwa ya Moyo wakati alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpa ushauri kuhusu afya ya Moyo Mzee John Lihame aliyembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiwaonyesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi upasuaji wa Moyo unavyofanyika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akijibu maswali mbalimbali kuhusu magonjwa ya moyo aliyoulizwa na wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wananchi hao walifika katika banda hilo kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fatuma Mkomwa akimpima mapigo ya moyo (BP) Mzee Mwanga ambaye alifika katika banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ally Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali wanazozitoa.
Neema Juma akimsikiliza kwa makini Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo wakati akimweleza namna anavyoweza kuishi na kuepukana na magonjwa ya moyo. Neema alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Wananchi wakiwa katika mstari wa kupima magonjwa ya Moyo bure na kupata ushauri katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tan trade Edwin Rutageruka (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi (katikati) alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Picha na JKCI

No comments: