Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano - Sekta ya
Mawasiliano, Injinia Angelina Madete amesema uanzishaji wa Taasisi ya
Teknolojia ya Ufundi (ICoT), utasaidia kupunguza pengo lililopo sasa
baina ya wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo hapa nchini.
Akifungua
warsha ya wataalam washauri na wadau wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi
Jijini Dar es salaam leo, Mhandisi Madete amewataka wataalam hao
kufanya uchambuzi wa kina ili kuwezesha taasisi hiyo mpya kukidhi
mahitaji ya mafundi sanifu na mchundo na hivyo kukidhi uwiano wa
kimataifa unaotaka mhandisi mmoja, fundi sanifu watano na mafundi
mchundo 25.
“Tunataka
kuwa nchi ya viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ni lazima tuwe
na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa kutosha
watakaofanyakazi kwa weledi na kumudu ushindani katika soko la ajira”,
amebainisha Injinia Madete.
Mhandisi
Madete amesema kuwa pengo la wahandisi, mafundi sanifu na mafundi
mchundo limeongezeka kutokana na vyuo vingi vya kati kutoa shahada hivyo
uwepo wa ICoT utakabiliana na kumaliza changamoto hiyo.
Aidha
amezungumzia umuhimu wa taasisi hiyo mpya kuanzisha kozi ya waendesha
mitambo ambayo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini na kwa sasa hakuna
chuo kinachotoa kozi hiyo.
Hakikisheni
taasisi hii inapata ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE), ili kuwawezesha wahitimu wote wa ICoT kupata fursa za
kujiendeleza na elimu ya juu.
Naye
mratibu wa wataalam wa uanzishaji ICoT Profesa Peter Chonjo amesema
wamejipanga kuhakikisha taasisi hiyo ya teknolojia ya ujenzi inakuwa ya
mfano hapa nchini kwa kuwa itawezesha wataalam wengi wa ujenzi kuwa na
weledi unaokubalika na kuibua uwezo wa ushindani katika soko la ajira na
hivyo kuwezesha Tanzania kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda
na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Tanzania
inakadiriwa kuwa na mtandao wa barabara wenye zaidi ya kilometa elfu 87
na kati ya hizo elfu 35 ni barabara za kitaifa na elfu 52 ni barabara
za Wilaya ambazo ujenzi wake unahitaji wataalam wa kutosha katika fani
ya ujenzi na uendeshaji wa mitambo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya
Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete akisisitiza jambo alipokuwa
akifungua warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi
(ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema
akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha
kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar
es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema
akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha
kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar
es Salaam leo.
Mmoja
wa wataalam elekezi wa uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi
(ICoT), Profesa Beatus Kundi akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya
ujenzi wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya
Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
– Sekta ya Ujenzi, Mhandisi John Ngowi (wa pili kulia) akifuatilia mada
wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya
Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya
Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya
Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete(wanne kutoka kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya ujenzi mara baada ya
kufungua warsha ya siku moja kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia
ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment