Monday, July 3, 2017

MBUNGE NYALANDU ATANGAZA DONGE NONO KWA BINGWA WA KOMBE LA NYALANDU CUP

Na,Jumbe Ismailly SINGIDA July,03,2017 Nyalandu 


MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu ametangaza donge nono kwa timu itakayokuwa bingwa wa mashindano ya kombe la Mbunge huyo,maarufu kwa jina la “NYALANDU CUP” linalotarajia kuanza mwezi wa nane mwaka huu.

Kombe hilo litakaloanza mwezi ujao,litashirikisha timu za mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa miguu kwa wanawake na kilele cha mashindano ya kombe hilo kitafanyika katika Kijiji cha Ngamu,kilichopo katika Kata ya Mwasauya.

Akitangaza msimamo wake huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour,Nyalandu alisema kwamba tangu alipochaguliwa kuwa mwakilisha wa wananchi wa jimbo hilo la Singida Kaskazini hajawahi kuandaa ligi ya aina yake kama hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezwa katika jimbo zima.

“Nilimwambia Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru nafikiri nilikuwa namnong’oneza kwamba mwenge ukipita na hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu nimekuwa Mbunge halafu kuchezesha mambo hii ya mechi”alifafanua ‘Mimi nafanyaaga maskolashipu,wasome sekondari,wafanye nini,mambo ya maji nafikiri sasa hivi tutaenda kwa zote, kwa hiyo ningependa kuanzisha ligi ambayo itafanyika ya mpira wa miguu lakini nataka iende sambamba na ligi ya wanawake” alisisitiza Mbunge Nyalandu.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo kutakuwa na ligi ya wanaume na itafungwa pamoja na ligi ambayo itakuwa ni ya wanawake na ligi hiyo watashirikiana kuitangaza,kuiunda na kuiandaa na serikali ya wilaya hiyo pamoja na Halmashauri hiyo kwa ujumla.

“Kwa hiyo itafanyika kwa uwazi kabisa na kwa wale wataalamu ambao ndiyo waandaa ligi watahusika katika kuiandaa kitaaalamu na mwisho wa ligi,mwisho wa yote na leo nilikuwa nimepanga tu kusema zawadi kwa upande wa mpira wa miguu”aliweka bayana Mbunge huyo wa jimbo la Singida Kaskazini.

Aidha Mbunge huyo hata hivyo pamoja na kutangaza zawadi kwa washindi wa mashindano hayo,vile vile alitangaza mapendekezo yake ya mahali patakapochezwa mchezo wa fainali ya ligi hiyo kuwa ni katika Kijiji alichokiita Kijiji pendwa cha Ngamu.

Akitoa sababu za mapendekezo hayo ya mchezo wa mwisho,Nyalandu alitanabaisha kwamba Kijiji cha Ngamu katika kata ya Mwasauya kutokana na kuwepo kwa mradi mkubwa wa Benki ya dunia wa kusambaza maji katika nyumba za watu.

“Halafu mshindi wa kwanza atapata zawadi,mshindi wa pili atapata zawadi na mshindi wa tatu atapata zawadi,ambapo kwa mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni tatu na kombe,jezi na mpira,mshindi wa pili zawadi shilingi milioni mbili,jezi na mpira na mshindi wa tatu zawadi shilingi milioni moja,jezi na mpira”aliweka bayana zawadi hizo kwa washindi.

Hata hivyo Nyalandu alitangaza pia zawadi kwa washindi wa mpira wa miguu wanawake kuwa ni shilingi milioni tatu kwa bingwa wa mashindano hayo,shilingi milioni mbili kwa mshindi wa pili na mshindi wa tatu shilingi milioni moja.

Naye Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaaifa mwaka huu,Amour Hamad Amour alishauri ushirikishwaji ufanyike ili kupata jina la ligi hiyo na hata hivyo hakusita kusisitiza kujittokeza kwa timu nyingi kushiriki katika mashindano hayo ili yawe mashindano ya kweli.
Mchezaji wa timu ya Mtinko Fc,Yusufu Samsoni (mwenye jesi yenye rangi ya bluu) alipomtoka mchezaji wa timu ya Msange Fc,Yasini Athumani na kwenda kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Msange FC wakifanya mazoezi katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Mtinko kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao matokeo yalikuwa Mtinko FC 2 na Msange FC 1.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

No comments: