Sensei Fundi Rumadha amefanya na kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do.
Hilo limejiri katika semina (Gasshuku) ya Masensei toka Ujerumani, Ureno, Uingereza, Japan, na Tanzania katika semina "Gasshuku" iliyofanyika jijini Warsaw, Poland, mwishoni mwa juma liliopita.
Sensei Rumadha sasa ana mamlaka ya kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania na kuwafanyia mitihani na kuwapa "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu katika Goju Ryu Karate kuanzia Dan ya 3 na kuendelea hutolewa na Master Miyazato pekee.
"Ni matumai yetu wanachama wa Jundokan So Honbu Tanzania kujiwajibisha kimafunzo, na kuimarisha umadhubuti wa mbinu (techniques) kuliko kulenga sana ngazi bila msingi mzuri kimafunzo, hasa katika kufanya "Kata" na "Bunkai". anasema Sensei Fundi Rumadha.
Sensei Rumadha, ambaye sasa anashikilia ngazi ya daraja la nne (Yondan) na mwenye uzoefu na umahili wa Goju Ryu Karate kwa zaidi ya miaka 38, alitoa Shukran zake kwa mlezi wake wa mafunzo tokea utotoni, Mwalimu "Sensei Magoma Nyamuko Sarya chini ya uongozi wake "Bomani Brigade" kama ilivyojilikana "BB" na mwanzilishi mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania mwaka 1973, hayati Sensei Nantambu Camara Bomani.
Tanzania na Angola zinatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato Sensei huko Naha City, Okinawa, mwezi wa Novemba 1918. Chama hicho kwa sasa kinaongozwa na mwanawe Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye pia ni Mwenyekiti mkuu dunia wa chama hicho na mwanae Master Eiichi Miyazato.
Sensei Miyazato amewafanyia mitihani ya mikanda myeusi zaidi ya walimu 15 toka ngazi ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nanadan". Ngazi hizi zote kwa utamaduni wa mtindo huu wa Okinawa Goju Ryu huchukua miaka mingi sana kupandishwa ngazi ambapo ni tofauti na mitindo mingine.
Kongamano la Karate mtindo wa Goju Ryu la Jundokan So Honbu hufanyika kila mwaka nchi za Ulaya kwa kutembelewa na wakuu wake toka katika visiwa vya Okinawa ili kuwasahihisha mbinu za mafunzo na mikakati mipya ya chama, na walimu toka nje ya bara la Ulaya kwa muda wa miaka zaidi ya miwili sasa ikiwemo Tanzania na Angola hualikwa.
Mwaka huu mitihani imefanyika kwa usimamizi wa walimu wakuu (Masters) watano chini ya mwenye kiti sensei Yoshihiro "Kancho" Miyazato, Tetsu Gima sensei, Tsuneo Kinjo sensei na Miyazaki sensei na mjumbe mwingine pia.
Wakuu hao wa Okinawa Goju Karate wametilia mkazo na msisitizo mkubwa sana kuzimudu mbinu kwa kina na matumizi yake, na pia kuandaa watoto wadogo kwani ndio walimu wa kesho.
Mengine juu la misafara hii ni kuwajumuisha masensei wote wa chama cha Jundokan So Honbu, kuwasahihisha na kuwafundisha mbinu za kupanda ngazi mbalimbali ili kupunguza gharama za kwenda Okinawa, Japan. kimafunzo.
Sensei Fundi Rumadha akikabidhiwa hati baada ya kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" toka kwa Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do ya Okinawa, Japan.
Sensei Fundi Rumadha akipongezwa kwan kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do.
Sensei Fundi Rumadha akiw na waamuzi toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato (katikati), ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do.
Masensei toka Ujerumani, Ureno, Uingereza, Japan, na Tanzania katika semina "Gasshuku" wakiwa na furaha nyingi baada ya kupandishwa daraja.
No comments:
Post a Comment