Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la
Mbulu Vijijini, Flatei Massay (wapili kulia) wakicheza ngoma ya
Wabarbaig/Watatoga kabla ya Masauni kuzungumza na mamia ya wananchi wa
Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la
Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la
Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo
ambayo inaishi pembezoni mwa mji wa Mbulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kabila
maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda
Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi
mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo iweze
kupata ulinzi wa kutosha katika eneo hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijadiliana na maafisa wa halmashauri ya
Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara pamoja na watendaji mbalimbali wa wilaya
hiyo, ndani ya jengo la mifugo lililopo Yaeda Chini katika makazi ya
Wahazabe, ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi. Kulia ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara (RPC), Francis Massawe, na
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwafafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la
Mbulu Vijijini, Flatei Massay (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini,
Zakaria Isaay mara baada ya Naibu waziri huyo kukagua Jengo la Mifugo
(nyuma yao) ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi ili
kuwasaidia wananchi wa kabila la Wahazabe na wengineo wanaoishi katika
Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kuleta ulinzi wa
raia hao pamoja na mali zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya
uhalifu ambayo yaliulizwa na wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha
Yueda Chini Wilaya ya Mbulu mkoani humo, ambalo kuna makazi ya jamii ya
Kabila la Wahazabe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wananchi wakimshangilia Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani) wakati alipowatangazia kufunguliwa Kituo cha Polisi hivi
karibuni katika Kijiji cha Bonde la Yueda Chini, lililopo wilayani
Mbulu, Mkoa wa Manyara. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………………………………………………..
Na Felix Mwagara (MOHA)
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Manyara
kufungua Kituo cha Polisi katika Makazi ya Kabila la Wahazabe wanaoishi
katika Bonde la Yueda Chini, wilayani Mbulu.
Masauni alisema hayo jana wakati
akizungumza na mamia ya wananchi wa kabila hilo mara baada ya kukagua
jengo la mifugo katika eneo la bonde hilo ambalo jamii hiyo ilijitenga
kwa kuweka makazi pembezoni mwa Mji wa Mbulu.
“Hivi karibuni Kituo cha Polisi
kitafunguliwa hapa ili kulinda usalama wenu katika eneo hili ambalo
lilikua halina kituo cha Polisi kwa miaka mingi. Serikali ya Rais
Magufuli ni sikivu ndio mana nimekuja hapa kuwasikiliza matatizo yenu na
kuwatekelezea.” Alisema Masauni huku akishangiliwa na wananchi hao.
Aliongeza kuwa, mchakato wa
kujenga kituo hicho umeanza na tayari ametoa maelekezo kwa Kamanda wa
Jeshi la Polisi wa Mkoa huo, kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu, Wabunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini na Mbulu Mjini.
Pia aliongeza kuwa, uhalifu
katika eneo hilo sasa umepata tiba kwa maana Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na wananchi watahakikisha hali ya usalama unaimarishwa
zaidi katika eneo hilo ambalo lipo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo
la Mbulu Vijijini, Flatei Massay alisema wananchi wa jimbo lake
wanavamiwa, wanaporwa mali zao ikiwemo mifugo, wanajeruhiwa na
wanaingizwa katika umaskini zaidi kutokana na waalifu kuwa wengi
kutokana na ukosefu wa Kituo cha Polisi.
“Nilimuomba na nilimsumbua sana
Naibu Waziri kule Bungeni ili aweze kufika katika eneo hili,
ninamshukuru sana kwa kufika na kutoa maelekezo ya kufunguliwa kituo cha
polisi, sasa wakazi wa eneo hili tunatarajia kupata ulinzi wa kutosha
baada ya kituo hicho kufunguliwa hivi karibuni,”alisema Massay.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani
humo, Francis Massawe alisema amepokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri
na mchakato utaanza rasmi na hatimaye kituo cha Polisi kitakuwepo
katika eneo hilo na wananchi wataendelea na shughuli zako za kutafuta
mahitaji yao kwa usalama zaidi.
No comments:
Post a Comment