Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na akiwa kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya
mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani
Kigoma, Dk. Jane Goodall.Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na
kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha
ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea kitabu kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe
kutoka kwa Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya
Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya
mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani
Kigoma, Dk. Jane Goodall. Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana
na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na Dk. Jane Goodall, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika
Ujumbe wake Dk. Goodall aliambata na Mama Getrude Mongela na Hadija
Simba ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Roots and Shoots pamoja na
watendaji wengine wa Taasisi hiyo.
Katika
mazungumzo yao Dk. Goodall pamoja na mambo mengine amezungumzia
uharibifu wa shoroba za wanyama pamoja na makazi yao katika hifadhi ya
Gombe iliyopo mkoani Kigoma ambayo ni maarifu kwa uhifadhi wa Sokwe.
Alisema kwa sasa hifadhi hiyo imezungukwa na maakazi ya binadamu hali
iliyosababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wanyama hao.
Aidha
Dk. Goodall alimuelezea Makamu wa Rais jitihada mbalimbali
zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kupambana na uharibifu wa
mazingira katika hifadhi ya Gombe ikiwemo kuhimiza uwepo wa mipango bora
ya matumizi ya ardhi.
“inawezekana
tatizo kubwa linalosababisha uharibu wa mazingira ni umasikini na
uelewa mdogo wa wananchi” alieleza Dk.Goodall. Hata hivyo alisema zipo
jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kutoa elimu
kwa umma.
Kwa
sasa wananchi kutoka katika vijiji zaidi 52 mkoani wa Kigoma wanapatiwa
elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Vilevile, jumla ya shilingi Milioni
400 zimekopeshwa kwa wananchi wa vijiji 32 ili kujiwezesha kiuchumi na
kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan yenye leno la
kulinda shoroba na makazi ya Sokwe. Hali hii imeanza kuleta mafanikio.
Dk.
Goodall ametaja changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ya Gombe
kuwa ni kuwepo kwa wakimbizi kutoka Burundi ambao kwa kiasi kikubwa
hushiriki katika shughuli ambazo husababisha uharibu wa mazingira kama
vile kilimo na ufugaji usio endelevu.
Kwa
upande wake Makamu wa Rais alisema serikali inafanya kazi kubwa katika
kuhakikisha mazingira ya hifadhi za Taifa pamoja na ikolojia yake
yanatunzwa. Makamu wa Rais amemhakikishia Dk. Goodall kwamba serikali
itaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakiksha wananchi wanafanya
shughuli za kujiletea maendeleo bila kuharibu mazingira.
“Ni
muhimu kuishirikisha jamii inayoishi pembezoni mwa hifadhi zetu katika
suala la uhifadhi wa mazingira lakini pia kuwa na mipango bora ya
matumizi ya ardhi”, alisema Makamu wa Rais. Kuhusu suala la wakimbizi
kuharibu mazingira, Makamu wa Rais aliahidi kutoa maelekezo kwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuona namna bora ya kulipatia ufumbuzi
suala hilo.
Mwisho,
Makamu wa Rais alimpongeza Dk. Goodall kwa kupewa tuzo ya heshima na
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama ishara ya kutambua mchango
wake katika masuala ya uhifadhi wa Sokwe na mazingira kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment