Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora
yatakayosaidia mamia ya wananchi nchini wanapata huduma za mawasiliano
ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mjini na vijijini.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua
Mkutano wa mwaka wa Chama cha Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE
360) Jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassana amesema anaimani kuwa wadau hao wa
makampuni ya simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha
mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia
wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini ambayo baadhi ya maeneo
hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.
“Ningependa
kusema kwamba Tanzania inakubali sana ushirikiano na GSMA na tunatamani
kupanua ushirikiano wetu na uwezeshaji kwa Watu wetu kwa njia ya sekta
ya simu ili kufikia utekelezaji wa ajenda za Maendeleo endelevu ya Umoja
wa Afrika AU na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020”.Amesisitiza
Makamu wa Rais.
Ameleeza
kuwa kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la
Afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia
simu za mkononi na kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na
baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki hivyo huduma hiyo
huwasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kutuma fedha kwa urahisi.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa
zaidi kwa huduma za kisasa za kimtandao ili wananchi waweze kunufaika
zaidi kwa njia hiyo katika sekta za elimu,afya, kilimo, biashara na
masuala ya kijinsia.
Amewahakikishia
wadau hao wa makampuni ya simu kuwa Serikali ya awamu ya Tano
itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha sekta hiyo
inaimarisha huduma zake kwa njia ya kisasa kwa wananchi.
Makamu
wa Rais amesema kuwa Serikali ya itaendelea kujifunza kutoka nchi
zingine ambazo zimefanya vizuri katika sekta ya mawasiliano ili taifa na
wananchi wake liweze kunufaika ipasavyo na huduma hizo kwa ajili ya
maendeleo endelevu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa
Makame Mbarawa amesema akizungumza katika mkutano huo ameeleza kuwa
Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Makampuni ya Mawasiliano
ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora
unaotakiwa.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam.
11-Julai-2017.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya
teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA
Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Baadhi
ya Wageni waalikwa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu
ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa
kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment