Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Makazi ya kulea Wazee cha Kolandoto Mkoani Shinyanga.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe jinsi ya kuwasha Jiko la Gesi lililopo katika kituo hicho ikiwa ni moja ya mradi wa majiko ya Gesi katika Makazi ya kulea wazee nchini wa pili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Rashid Mfaume.
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe akiwasha moja ya Jiko la gesi lililopo katika kituo chake wakati Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (kushoto) alipotembele kukagua maendeleo ya mradi huo hivi karibuni.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(Kushoto) akiangalia moja ya jiko linalotumia Nishati ya Gesi linalowaka wakati alipotembele kukagua maendeleo ya mradi huo hivi karibuni.
Muonekano wa Majiko yanayotumia Nishati ya Gesi yatakayotumiwa kuhudumia katika makazi ya kulea wazee ya Kolandoto na makazi mengine ya kulea wazee nchini.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akizungumza na Mwenyekiti wa wazee waishio katika makazi ya Kolandoto Shinyanga Mzee Maganga alipotembelea kujionea maendeleo ya ujenzi kabla ya kuwekwa kwa jiwe la Msingi katika jingo la bweni la wazee n maradi wa majiko yanayotumia Nishati ya Gesi.
Picha na Raymond Mushumbusi WAMJW
No comments:
Post a Comment