Tuesday, July 11, 2017

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAKABIDHIWA GARI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akisalimiana na Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Iringa, mara baada ya kuwasili katika sherehe za makabidhiano ya gari la kuzimia moto lililotolewa na Mdau Ndugu, Zakaria Hanspoppe kwenye kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo mapema leo asubuhi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakitoa salamu ya heshima kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi katika shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la ZImamoto na Uokoaji mara baada ya kuwasili kituoni hapo mapema leo asubuhi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni ambaye ameketi meza kuu katikati. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mdau Ndugu Zacharia Hanspoppe (wa kwanza kushoto) ambaye ndiye aliyetoa msaada wa gari la kuzimia moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akitoa pongezi kwa Viongozi wa Jeshi hilo kwa jitihada wanazofanya katika kukabiliana na majanga ya moto, mafuriko, ajali za barabarani na majanga mengine. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi gari la kuzimia moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio ambalo limeshuhudiwa na Kamaishna Jenerali wa Jeshi hilo, Viongozi mbalimbali wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani humo, Mdau aliyetoa msaada huo Ndugu, Zacharia Hanspoppe, Maafisa na Askari wa Jeshi hilo pamoja na wananchi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akionesha funguo ya gari hilo mara baada ya tukio la kukata utepe na kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Bi. Amina Masenza ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza mwenye kitambaa cheupe katikati, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wa kwanza mbele, Mdau ndugu Zachalia Hanspope wa pili kutoka kushoto, pamoja na Viongozi wa kamati ya vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani Iringa wakifurahi tukio la makabidhiano. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Gari lililokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoro na Uokoaji Thobias Andengenye. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) mara baada ya kuhitimisha shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto lililotolewa msaada na mdau Ndugu Zacharia Hanspoppe. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).

No comments: