Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la
kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa
msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.
Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa
Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh.
Geofrey Ngupula ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho
kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea
wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma
stahiki.
Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk.
Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi
wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi
hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa
msaada kwa kuwapeleka wateja katika
ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali za Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.
Aidha, alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yoyote ile, gari
hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo
za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo.
“Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote pamoja na dereva.
Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa
linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio
kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo
Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu” alieleza Mh.
Ngupula.
Ameongeza kuwa gari hilo ambalo ni la kisasa, litunzwe na
kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo na kuwa msaada kwa Tarafa hiyo na wananchi wote
watakaopata msaada.
Kwa upande wake, Dk. Kigwangalla amewaomba wananchi
waendelee kumuombea kwa kazi anayofanya ikiwemo jukumu la kulitumikia Taifa
katika nafasi yake ya Unaibu Uwaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
Dk. Kigwangalla ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini
ya Rais Magufuli kwa kuweza kuwa karibu
na Wananchi ikiwemo kushughulikia suala la maji kutoka Ziwa Victoria na kuja
Mkoa wa Tabora ikiwemo kuanzia katika Wilaya hiyo ya Nzega na kisha kwenda
maeneeo mengine.
“Tunampongeza Rais wetru Dk. Magufuli kwa kuwa karibu na
wananchi wake. Tulikuwa nae Mkoani kwetu hapa Tabora na amezindua miradi
mbalimbali ikiwemo ya barabara na ule wa maji safi yatakayotoka Ziwa Vitoria.
Shida ya maji kwa wananchi wa Nzega inaenda kuwa histoa kwani Maji hayo
yatakuja hapa na kisha kwenda maeneo mengine. Rais wetu anatupenda na tuendelee
kumuunga mkono hasa juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi yetu na pia
katika kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi wa Taifa letu
Mimi Mbunge wenu pia muendelee kuniombea na kila siku mawazo
yangu na akili yangu ipo pamoja nanyi ndio maana nimeweza kuwaletea gari hili
la wagonjwa, na pia kufanikisha kuandaa kambi maalum ya matibabu bure ya wiki
moja kwa wananchi wote wa Nzega bure” alieleza Dk. Kigwangalla.
Tukio hilo la ukabidhi wa gari hilo pia lilishuhudiwa na
viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Jimbo hilo na wale wa jimbo jirani
ikiwemo Bukuene, Viongozi wa ulinzi na Usalama pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Nzega.
No comments:
Post a Comment