Friday, July 14, 2017

AZAM YAENDELEA NA MAKAMUZI YA MAANDALIZI YA LIGI KUU MSIMU UJAO


Kikosi cha timu ya Azam kimeanza mazoezi ikiwa  ni maalumu kabisa katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu ujao, ambapo Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amepanga kutengeneza kikosi kikali kitakachoweza kufanya makubwa katika siku za usoni.

Kikosi hicho leo kimeshafanya mazoezi mara mbili, saa 1.00 asubuhi na 3.30 asubuhi na kitamalizia mazoezi mwisho saa 11.00 jioni ndani ya viunga vya Azam Complex, Chamazi.

Cioaba amesema faida kubwa ya kufanya mazoezi makali hivi sasa ni kuwajenga wachezaji kwenye maeneo mbalimbali, kiufundi uwanjani, stamina na ustahimilivu kwenye kupambana.

Baada ya kumaliza programu hiyo ya mazoezi, Azam FC itasafiri Julai 20, mwaka huu kuelekea kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikienda kucheza mechi tatu za kirafiki, ya kwanza ikiwa ya mwaliko dhidi ya Mbeya City, itakayofanyika Julai 22 katika siku watakayokuwa wakisherehekea Mbeya City Day.

Mechi nyingine za kirafiki itacheza na timu mbili zilizopanda daraja. Njombe Mji Julai 24 mwaka huu mjini Njombe na ikimaliza ziara hiyo kwa kukipiga na Lipuli ya Iringa Julai 26 kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Julai 27.

 Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi leo asubuhi ikiwa ni katika maandalizi ya msimu ujao chini ya  Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba na Iddy Cheche. 


Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi ya viungo leo asubuhi ikiwa ni katika maandalizi ya msimu ujao chini ya  Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba. 



No comments: