Monday, June 12, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAVALISHA VYEO MAAFISA WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS,AHIMIZA HAKI NA USAWA MAGEREZA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Magereza kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa mahaliwa alimwakisha Rais John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.  Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla  hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
Manaibu Kamishina wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aktika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya kuvalisha vyeo Maafisa magereza iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 

           
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.

Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa 24 kuwa Kamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo Mei 25, mwaka huu.

“Ninyi ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.

Waziri Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu, mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na uadilifu mkubwa,” amesema.

Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Yusuph Masauni amewataka maafisa waliovishwa vyeo wazingatie maadili ya kazi zao na uzalendo kama ambavyo wameapa kwenye kiapo cha maadili.

Maafisa watano waliovalishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni SACP Uwesu Ngarama; SACP Gideon Mkana (Mkuu wa Chuo cha TCTA); SACP Jeremiah Nkondo (RPO-Kagera); SACP Tusekile Mwaisabila (RPO-Lindi) na SACP Augustine Mboje (RPO-DSM).

Maafisa 24 waliovalishwa vyeo kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP) ni ACP Mbaraka Semwanza; ACP George Mwambashi; ACP Charles Novati; ACP Faustine M. Kasike; ACP Joel Bukuku; ACP Deogratius Lwanga; ACP Boyd P. Mwambingu (RPO Pwani); ACP Athumani Kitiku (RPO Mwanza) na ACP Hassan Mkwiche (RPO Kilimanjaro).

Wengine ni ACP Luhende D. Makwaia; ACP Hamza R. Hamza; ACP Jeremiah Y. Katengu; ACP Mzee R. Nyamka (Kaimu RPO Morogoro); ACP Afwilile Mwakijungu (Mkuu wa gereza la Isupilo, Iringa); ACP Ali Kaherewa (Kaimu RPO Singida); ACP Ismail Mlawa (RPO Mtwara); ACP Chacha B. Jackson; ACP Rajab N. Bakari; ACP Kijida P. Mwankingi; ACP Julius C. Ntambala; ACP Mussa M. Kiswaka; ACP Justin Kaziulaya na ACP Bertha J. Minde.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JUNI 12, 2017.

No comments: