Tuesday, June 6, 2017

WANAOLIMA KWENYE MAENEO OEVU WAONDOKE- RC MASENZA



Mhifadhi mwandamizi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Moronda Moronda akitangaza washindi wa tuzo za uhifadhi mazingira za TANAPA .

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah wakimpongeza mwakilishi wa kikundi cha familia ya Festo Mhanga wa Kilolo kwa kushinda tuzo ya Mazingira ya Tanapa na kuzawadiwa shilingi milioni jana wakati wa kilele cha siku ya Mazingira na utoaji wa Tuzo za TANAPA kwa wananchi wa mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya


Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira duniani jana Amos Makala mkuu wa mkoa wa Mbeya akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na meneja ujirani mwema wa Tanapa Ahmed Mbugi kushoto .

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa salam siku ya Mazingira Duniani mkoani Mbeya .

Kikundi cha skauti cha elimisha jamii wilaya ya Mufindi wakikabidhiwa hundi ya shilingi milioni 1 toka Tanapa

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akitoa salam siku ya mazingira duania

Na matukiodaimaBlog


SERIKALI Imewataka wananchi wanaolima kilimo kwenye maeneo oevu maarufu kama vinyungu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya nje ya kilimo hicho kulinda mto Ruaha mkuu kukauka.

Akitoa salam za mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya tuzo ya TANAPA ya uhifadhi mazingira na kilele cha siku ya mazingira Duniani leo maadhimisho yaliyofanyika kwa kijiji cha Madabaga wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya Jana mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema iwapo ulimaji wa vinyungu utafumbiwa macho mto Ruaha mkuu utaendelea kukauka.

Alisema kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya mto Ruaha mkuu pamoja na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Kwani alisema uhifadhi wa hifadhi ya Ruaha ni pamoja na uhifadhi wa mto Ruaha mkuu hivyo mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wana wajibu wa kulinda mto Ruaha mkuu na kuchukua hatua kwa wote wanaolima kwenye vyanzo vya maji.
Wakuu wa wilaya ya Mbeya na Mufindi wakijadili jambo

Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira duania Amos Makala mkuu wa mkoa wa Mbeya na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na viongozi wengine wakiwasilia uwanja wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani

Masenza alisema wajibu wa kulinda mto Ruaha mkuu upo mikononi mwa viongozi wote wakianza wale wa serikali za vijiji." Niwaombe sana wananchi wote tuungane kulinda mto Ruaha na jambo hili uwe ni utamaduni wetu na halihitaji suluti "

Mhifadhi mwandamizi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Moronda Moronda alisema kwa siku ya mazingira ambayo ni mwaka wa pili kufanyika mikoa ya Njombe,Mbeya na Iringa huambatana na tuzo kwa vikundi na mtu mmoja mmoja anayefanya vema katika uhifadhi.

Alisema kwa mwaka jana ndipo zoezi la utoaji tuzo lilianzishwa kwa kuwa na washiriki 200 ila idadi ya washiriki kwa mwaka huu imeingezeka hadi kufikia washiriki zaidi ya 500.

Maronda alisema kuwa uharibifu wa ikolojia ya mto Ruaha mkuu umeendelea kuharibiwa na urejeshaji wa mto unaoharibiwa gharama yake ni kubwa zaidi.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala alisema kimataifa maadhimisho hayo yamefanyika nchini Canada na kitaifa yamefanyika mkoani Mara.

Hivyo alisema maendeleo ya uchumi wa nchi uende sambamba na uhifadhi wa mazingira na kuwa suala la uchomaji ovyo pamoja na kilimo kisichoendelevu hakitavumilika.

Alisema tayari makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kunusuru ikolojia ya mto Ruaha mkuu hivyo viongozi wote wanapaswa kusimamia Sheria zilizopo na kuepuka siasa zinazochangia uharibifu wa mazingira.

" Hivyo nawaomba sana viongozi na wananchi wote kusimamia sheria kwa kutoa elimu na kazi ya kusimamia sheria inatupaswa tuifanye sisi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya maana sisi hatupigiwi kura.

Hivyo alisema njia pekee ya kulinda mazingira ni kupanda miti kwa kila wilaya miti milioni 1.5 na kwa kila mkoa miti milioni 15.

Kuhusu mifugo kuongezeka alitaka senza ya mifugo kufanyika na baada ya hapo ng,ombe zote zitapigwa chapa kuitambua na mifugo iliyopo katika hifadhi kama Ihefu kuondolewa haraka.

No comments: