Thursday, June 1, 2017

WANAHABARI, WATAFITI WA KILIMO KUTOKA NCHI TANO ZA AFRIKA WAAGANA HOTELI YA MALAIKA BEACH RESORT JIJINI MWANZA

Na Dotto Mwaibale, Mwanza
WAANDISHI wa Habari na Watafiti wa kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na Tanzania wameagana katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana baada ya kumaliza ziara ya utoaji wa mafunzo kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Buchosa Sengerema.
Hafla hiyo iliandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima Wadogo (AATF).
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na (OFAB) kwa kushirikiana na  (AATF) yalikuwa na lengo la kuwakutanisha waandishi wa habari na wataalamu wa kilimo kutoka katika nchi hizo waweze kukutana na kupeana uzoefu wa jinsi ya kuandika habari za kilimo kwa kutumia Bioteknolojia.
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo ya namna hiyo yataendelea kutolewa ili kuwajengea uwezo wanahabari wanaoandika hababari za kilimo ili waweze kuandika habari hizo kwa ufanisi bila kukiuka maadili.

"Tutaendelea kuwawezesha wanahabari wanaoandika habari za kilimo ili wawe na uwezo wa kuandika habari za kilimo kwa weredi mkubwa" alisema Nyinondi.
 Mwanahabari Lucy Ngowi (kushoto), akichangamkia mapochopocho katika hafla ya kuagana kati ya wanahabari kutoka nchi tano za Afrika na wataalamu wa kilimo kutoka katika nchi hizo baada ya kumaliza ziara ya utoaji wa mafunzo kwa maofisa ugani wa Wilaya ya Chato mkoani Geita na Buchosa Sengerema hafla iliyofanyika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana usiku. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima Wadogo (AATF). Kutoka kulia ni Ofisa kutoka idara ya Fedha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mr Nyamka na dereva wa Costech Mr. Nasibu.

 Mr. Nyamka na dereva Mr. Nasibu wakiwa katika makulaji wakati wa sherehe hiyo.
 Hapa ni kujiachia kwa kwenda mbele.
 Wanahabari kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia na Burknafaso wakiserebuka hapo wimbo kutoka Ethiopia upkipigwa na huyo jamaa aliyeinua mikono juu kwa mzuka ni mwanahabari kutoka Ethiopia akifurahia mziki wa kwao.
 Hapa ni furaha tupu. Kushoto ni mwanahabari kutoka Uganda na wapili kushoto ni mtaalamu wa kilimo na mtafiti kutoka Jukwaa la Bioteknolojia nchini Burknafaso, Dk. Traore.
 Wanahabari na watafiti wakifurahi katika hafla hiyo.
 Watafiti wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge, Mshauri Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Mahindi Yanayostahimili Ukame Afrika (WEMA) Tawi la Tanzania Dk.Alois Kulaya na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange.
 Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Mahindi Yanayostahimili Ukame Afrika (WEMA) Tawi la Tanzania Dk.Alois Kulaya (kulia), akiongoza kusakata rhumba kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi waa Habari za Kilimo (TAJF), Gerald Kitabu.
Mserebuko ukiendelea.



No comments: