Saturday, June 24, 2017

WAFANYA BIASHARA WASIOTUMIA MASHINE ZA EFD WAFUNGIWA MADUKA NA TRA KARIAKOO

Maafisa wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA) wameendelea  kufanya zoezi la ukaguzi wa maduka ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao pasipo kuwapatia risiti za mashine za Kielektroniki (Efd) jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeendelea kufanyika katika eneo la Kibiashara la Kariakoo na itakuwa endelevu kuhakikisha wafanya biashara wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za biashara katika mauzo ya bidhaa zao. 
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart na askari polisi wakisimamia zoezi la kuingiza ndani bidhaa za wafanya biashara walikutwa wakiendelea kutoa huduma ilhali awali walikutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine. Hatua ya ukamatwaji kwa wafanya biashara hao inatokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)
Add caption
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart akifunga kofuli la wafanyabiashara walikamatwa katika Mtaa wa Aggrey Kariakoo Dar es Salaam wakifanya biashara bila pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine hiyo. Hatua ya kuwakamata wafanya biashara hao imetokana na kushindwa kuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Hivyo basi watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart akifunga kofuli kwenye lango duka la wafanya biashara waliokamatwa katika Mtaa wa Aggrey Kariakoo Dar es Salaam wakifanya biashara bila pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine. Hatua ya kuwakamata wafanya biashara hao imetokana na kushindwa kwao  kuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
Afisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini (kushoto) akisubiri mmiliki wa duka la urembo  lililokutwa likiendelea kufanya biashara hata baada ya kukutwa wakiuza bidhaa zao pasipo kutoa risiti za kielekroniki licha kuwa na machine inayotakiwa kutumika kwa utoaji wa risiti kwa wateja wao iliyotolewa na TRA. Hatua ya kuwakamata wafanyabiashara hao imetokana na kitendo cha uongozi wa duka hilo kutokuitikia wito wa TRA kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Wafanya biashara hao watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
Wafanya biashara waliokamatwa eneo la Kariakoo Mtaa wa Congo Dar es Salaam, kwa kosa la kutoitikia wito wa mamlaka hiyo kwenda kulipia faini ya utoaji wa huduma pasipo kutoa risiti za kielektoniki licha ya kuwa na mashine wakifunga duka lao walipokamatwa na maofisa wa TRA Juni 22 2017. Kwa mujibu wa sheria za nchi wafanyabiashara hao watatakiwa kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart (kulia) na mmoja wa wafanya biashara wakifunga makofuli kwenye duka la madera katika mtaa wa Congo Kariakoo Dar es Salaam Juni 22 2017 baada ya kukutwa duka hilo likiendelea kutoa huduma ilhali awali walishakutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine ya risiti za kieletroniki (Efd). Hatua ya kuwakamata wafanyabiashara wa jinsi hiyo ilitokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.

 

No comments: