Friday, June 9, 2017

TASWIRA MBALIMBALI ZA MATUKIO MAHAKAMA- KANDA YA IRINGA

 Kaimu Hakimu Mkazi-Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Njombe, Mhe. Paul Kapokolo akiwa ofisini kwake mkoani Njombe, Mhe. Kapokolo ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya Njombe amesema Mahakama mkoani Njombe imejiwekea mikakati ya kushughulikia mashauri kwa wakati ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya kusukuma mashauri (case flow management) ili kupata ufumbuzi kwa mashauri yanayoonekana kukwama, kuhimiza Waendesha Mashitaka/Polisi kuleta mashahidi kwa kila tarehe wanayopangiwa kusikiliza mashauri n.k
 Mtendaji, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Njombe, Bi. Maria Francis Itala, Bi. Itala alisema kuwa Mahakama mkoani Njombe wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa Watumishi wa Kada mbalimbali, alisema kwa sasa Mkoa huo una jumla ya Watumishi 78 na uhitaji wa Watumishi ili kutekeleza Majukumu tofauti tofauti ni 359, na hivyo kufanya kuwa na upungufu wa Watumishi 28.
 Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Makambako lililopo mkoani Njombe, hali ya miundombinu ya Majengo katika mkoa huu inaridhisha kwa wastani ingawa kuna baadhi ya maeneo ambayo majengo yake yanahitaji kufanyiwa ukarabati au kujengwa kutokana na kutokuwepo kwa majengo kabisa.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey (kushoto) akiwa katika ukaguzi maalum alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Kalenga-Iringa ili kujionea hali ya utendaji kazi katika Mahakama hiyo.
 Moja ya vitu alivyokagua Hakimu huyo Mfawidhi, Mhe. Kalenga ni pamoja na Rejesta ya Mahakama ya Mwanzo Kalenga kuangalia kama rekodi zinajazwa vizuri kulingana na aina ya kesi zinazofunguliwa.
 Jengo la Mahakama ya Mwanzo Kalenga- Iringa ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya-Iringa amefanya ukaguzi
 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakma ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya alipomaliza kusaini kitabu cha wageni pindi alipowasili katika Mahakama ya Mwanzo Kalenga kwa ajili ya ukaguzi wa Mahakama hiyo.
 Mhe. Isaya, wa kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo-Kalenga, wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Mwanzo-Kalenga, Mhe. Magdalena Malaba.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Kalenga mara baada ya kukamilisha shughuli ya ukaguzi iliyompeleka katika Mahakama hiyo. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)

No comments: