Friday, June 9, 2017

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAWAPIMA AFYA VIONGOZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaelezea wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka wakati wafanyakazi hao walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Fatuma Chillo akiuliza ni muda gani mzuri wa kupima shinikizo la damu mwilini (BP) wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya upimaji wa afya zao. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Katibu wa NHC Martin Mdoe.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Fatuma Chillo akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimpima urefu na uzito Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba wakati viongozi wa Taasisi hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimpima shinikizo la damu (BP) Meneja Uendeleza Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Haikamen Mlekio wakati viongozi wa Taasisi hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Tabora Dickson Ngonde akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo, tezi dume na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimpima shinikizo la damu (BP) Meneja Oparesheni za Mikoa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Maneno Mahenge wakati viongozi wa Shirika hilo walipofika JKCI leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Peter Issack akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo, tezi dume na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao. Picha na JKCI

No comments: