Monday, June 19, 2017

SPRITE BBALL KINGS YAINGIA HATUA YA MTOANO, DROO KUCHEZWA LEO USIKU

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi kwa michezo mitano kupigwa katika uwanja wa Habours Club Mivinjeni na kufanikisha kupatikana kwa timu zitakazoungana na zingine za wiki iliyopita.

Hiyo ni raundi ya pili ya mashindano hayo ikiwa ni muendelezo wa michezo ya mtoano iliyoanza takribani wiki tatu zilizopita ili kumpata bingwa wa Sprite BBall Kings 2017.
Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na Ukongana timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 za Ukonga.

Mechi ya pili iliwakutanisha Ardhi ambaye alitoka na ushindi wa vikapu 60 dhidi ya Heroes B aliyepata vikapu 42, Flying D wakaumana na UDSM na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 68 dhidi ya vikapu 45.

Mechi ya nne iliwakutanisha Kigamboni na St Montfort na ulimalizika kwa vikapu 71 vya Kigamboni dhidi ya 40 vya Montfort huku mechi ya mwisho ikiwa ni DMI aliyetoka na vikapu 41 dhidi ya 74 vya Oysterbay na kuhitiMisha michezo ya raundi ya pili ya Sprite Bball Kings.

Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wiki hii kutachezeshwa kwa droo maalumu kwa ajili ha kuzipanga timu zitakazochuana kwenye hatua ya mtoano ya raundi ya tatu ya Sprite BBall Kings 2017.

"Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya wiki iliyopita na katika michezo ya ju ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya michuano ya Sprite BBall Kings na kutakuwa na droo ya moja kwa moja itakayorushwa hewani kupanga timu zitakazoumana,"amesema Basilisa.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio huku mshindi akitarajiwa kuondoka na kitita cha shiling milion 15. 

Timu ya Mchenga (Njano) wakiumama katika hatua ya pili ya michuano ya Sprite BBalla Kings dhidi ya Ukonga katika mechi iliyopigwa Harbours Club Mivinjeni na Mchenga kutoka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63. 

Timu ya Kigamboni Heroes (wekundu) wakisalimiana na St Montfort kabla ya mchezo wao wa hatua ya pili ya Sprite BBall Kings uliofanyika katika uwanja wa Harbours Club Mivinjeni na Kigamboni kuibuka na ushindi wa vikapu 71 dhidi ya 40
 Mohamed Yusuph mchezaji wa Mchenga akipiga pigo la adhabu kwa timu yake katika mchezo wa hatua ya pili ya michuano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa Mchenga kupata ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 vya Ukonga.

No comments: