Thursday, June 22, 2017

SIMU TV: Habari kutoka televisheni

Simu.tv: Rais Dr John Pombe Magufuli amesema serikali haitawaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni kuendelea na masomo. https://youtu.be/Dn82AeasiaY

Simu.tv: Nyumba 13 katika kijiji cha Bugasha wilayani Muleba zimeteketezwa kwa moto kwa siku tofauti huku chanzo cha moto huo wa ajabu hakijajulikana. https://youtu.be/OvLEXSvGcxw

Simu.tv: Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatoa huduma za viwango kwa wakati ili kukuza uwazi na uwajibikaji kwa kila mtu katika taasisi zake. https://youtu.be/EXNLicAB7Cg

Simu.tv: Wananfunzi watatu walioshinda medali za dhahabu kwa kila mmoja katika mashindano ya kimataifa ya mazingira wamerejea hapa nchini. https://youtu.be/Cir7RqBASvQ

Simu.tv: Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira January Makamba amezitaka halmashauri kuanisha maeneo yenye vyanzo vya maji na kuweka mpango sahihi wa matumizi. https://youtu.be/LBAX0zYQUpQ

Simu.tv: Bunge limepitisha muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2017 kwa lengo la kuhalalisha kisheria utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018. https://youtu.be/9u57HeSZxvU

Simu.tv: Wakazi visiwani Zanzibar wameshauriwa kuendelea kunywa maji ya dafu ili kupata faida zitokanazo na maji hayo. https://youtu.be/pj-Vhds7aWM

Simu.tv: Waziri mkuu Kasimu Majaliwa ameziagiza halmashauri zote nchini kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini kuthibiti ukwepaji wa kodi. https://youtu.be/du6BK72rNZg

Simu.tv: Washiriki wa maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba wametakiwa kujifunza kutoka kwa washiriki wa  kimataifa ili kuboresha bidhaa wanazo zalisha. https://youtu.be/Kj8PjdyTshs

Benki ya CRDB imezindua dirsha jipya kwa wawekezaji wa kitanzania wenye nia ya kuwekeza katika mashamba makubwa na uanzishaji wa viwanda ili kutekeleza azma ya kufika Tanzania ya viwanda. https://youtu.be/QTrsMhsq4A8

Simu.tv: Kikosi cha wachezaji 22 cha timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars kimeondoka kuelekea nchini Afrika Kusini kushiriki michuano ya COSAFA ambapo taifa stars inashiriki kama mgeni mwalikwa. https://youtu.be/WIP7JWoXZSM

Simu.tv: Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF imetangaza kuwa uchaguzi wa viongozi kwa chama cha soka mkoa wa Rukwa RUREFA utafanyika tarehe tano mwezi August. https://youtu.be/1yEBcBnru04

Simu.tv: Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Pope amesema mchezaji wa zamani wa timu hiyo Emanuel Okwi atatua nchini kusaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo. https://youtu.be/X1nuRHnfO94

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa kukosekana kwa ofisi ya TRA wilayani Chato mkoani Geita kumeikosesha serikali mapato; https://youtu.be/rReuPe3-z9s

SIMU.TV: Waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya mazingira January Makamba ameagiza kuthibitiwa kwa watendaji wasiosimamia utunzaji wa mazingira; https://youtu.be/aNq86jBZVrE

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Stephen amemuagiza katibu tawala wa mkoa huo kumsimamisha kazi kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Nkasi kwa sababu ya uzembe; https://youtu.be/M74ZxnMka7c

SIMU.TV: Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar Es salaam imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa taasisi ya Kiislamu ya Mico kusaidia huduma za afya; https://youtu.be/eIrl_52gUm8

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini Tanzania TRA imeendesha operesheni ya kuwafungia maduka wafanyabiashara wasiotoa risiti kwa wateja sokoni Kariakoo; https://youtu.be/p6eKhwCboVM

SIMU.TV: Washiriki wa maonyesho ya 41 ya kibiashara maarufu kama Sabasaba wameshauriwa kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wa kigeni ili kuboresha bidhaa zao; https://youtu.be/HRnuODePpho

SIMU.TV: Watanzania wanaotaka kuanzisha viwanda nchini wametakiwa kutumia huduma za kifedha ili kuweza kufikia Tanzania ya viwanda; https://youtu.be/37u5XJuedVQ

SIMU.TV: Mkurugenzi wa utafiti wa masoko wa benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa amesema kuwa benki hiyo imetumia zaidi ya shilingi Trilioni 1.84 kwenye miradi ya maendeleo; https://youtu.be/b_f03kmQrn8  

SIMU.TV: Aliyekuwa shabiki wa klabu ya Yanga maarufu kama Ally Yanga amepumzishwa leo katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao mkoani Shinyanga; https://youtu.be/W7zatvS7N3s

SIMU.TV: Kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema uteuzi wa kikosi chake una malengo maalumu kulingana na aina ya mashindano waliyonayo; https://youtu.be/PjoNqTCi0xo

SIMU.TV: Wanariadha wa Tanzania wanaokwenda kushiriki michuano ya kimataifa wametakiwa kuepukana vikali na matumizi ya dawa za kusisimua misuli; https://youtu.be/wU2CE1bHbqQ

SIMU.TV: Wanafunzi 15 kutoka katika shule ya sekondari ya Feza wameibuka kidedea katika mashindano ya vipaji huko nchini Marekani kwa kujinyakulia medali za dhahabu; https://youtu.be/J1qtnknpYQ8

SIMU.TV: Kuelekea sikukuu ya Eid El Fitr wasanii Roma, Stamina na Snura wameungana kwa ajili ya kuangusha burudani kali katika viwanja wa Dar live Mbagala; https://youtu.be/4_HvgWIGTRM

No comments: