Wednesday, June 7, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Kuelekea uwasilishwaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2017/2018 wabunge wameishauri serikali kubuni njia mbadala za upatikanaji wa mapato. https://youtu.be/-Uel22rXuCA

SIMU.TV: Chama cha ACT wazalendo kimempongeza rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kumteua aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Anna Nghwira kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. https://youtu.be/tcrLLUEzZm0

SIMU.TV: Serikali mkoani Mtwara imesema itahakikisha kila aliyechukua fedha za wakulima katika msimu wa korosho uliopita wanazirejesha kabla ya msimu ujao kuanza. https://youtu.be/46Erk-2f53Q

SIMU.TV: Mamlaka ya uthibiti wa nishati na maji EWURA imesema wadau wanaalikwa kutoa maoni yao kuhusu mkataba wa uzalishaji wa umeme wa kampuni ya IPTL kabla ya kutoa leseni mpya kwa kampuni hiyo. https://youtu.be/AFmjp1op1I8

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameshauri kufanyiwa kwa marekebisho ya sheria inayowaruhusu wahamiaji kupata vibali na kufanya vibarua katika wilaya hiyo. https://youtu.be/M5jSVSa_Ewc

SIMU.TV: Askari wastaafu waliopigana katika vita kuu ya pili ya dunia wamempongeza rais Magufuli kwa juhudi anazochukua kuzuia wizi wa rasilimali za watanzania. https://youtu.be/is4TbH0hNS0

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ametoa karipio kali dhidi ya wanaume wanaowarubuni wanafunzi wa kike na kuwapa mimba na kusema yeyote atakayebainika hatabaki salama. https://youtu.be/rf_dIwnCVqM

SIMU.TV: Baadhi ya wamiliki wa maduka ya jumla ya bidhaa za vyakula katika halmashauri ya mji wa Nzega wamegoma kufungua maduka yao wakilalamikia kero ya ushuru wa huduma unaotozwa na halmashauri hiyo. https://youtu.be/hsIPHwFRKBg

SIMU.TV: Wafanyabiashara wenye maduka katika eneo la kariakoo jijini Dar es Salaam wamelalamikia vitendo vya Machinga kupanga bidhaa maeneo ya maegesho ya magari na mbele ya maduka yao. https://youtu.be/Tx1ggvB3egY

SIMU.TV: Wanawake wajasiriamali wanaotengeneza kamba zitokananzo na makumbi ya nazi visiwani Zanzibar wamesema mauzo yameshuka katika kipindi hiki ambacho sio cha utalii. https://youtu.be/nCW0HKAnKR8

SIMU.TV: Timu ya taifa ya soka Taifa Stars imerejea nchini leo ikitokea nchini Misri ilikokuwa imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Lesotho utakaochezwa jumasosi. https://youtu.be/t78iRm6_slU

SIMU.TV: Jeshi la kujenga taifa JKT limeazimia kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya michezo kujiunga na jeshi hilo kwa ajili ya kupata mafunzo ya jeshi hilo. https://youtu.be/HwTZya1zaxw

SIMU.TV: Klabu ya Manchester United imeongoza katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa zaidi duniani na hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes. https://youtu.be/BQiIXTe7Juk

No comments: