Friday, June 23, 2017

RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA VITANDA,MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA LEVOLOSI

 Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha  Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 Picha ikionyesha  wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum(CCM)Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais  John Magufuli    msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda  25 katika  kituo cha afya cha Levolosi  ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni  ,katikati ni Mganga  mkuu wa kituo cha Afya cha Levolosi  Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha (picha na Woinde Shizza,Arusha)
 Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo
 Mkuu  wa wilaya ya Arusha  Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi  wa jiji la Arusha


 Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo
   Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji  mara baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo
Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda ,mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)

 Na Woinde Shizza,Arusha.
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitihada za maendeleo ambazo zinafanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitiada hizo zinamanufaa makubwa kwa wananchi.

Aidha  kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya   Rasi kitu  ambacho sio kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema

 Hayo yamesemwa   leo jijini hapa  na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha  Catherine Magige  wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi  vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

Alisema k uwa  kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi  za Rais na kusema kuwa  afanyikitu chochote 

"Rais  wetu anafanyakazi mtu anaesema afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili angalieni jinsi alivyozuia makontena  ya madini,angalieni jinsi alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu wawananchi wa mkoa wa Arusha na  ameamua kutoa msaada wa  magodoro ,mashuka pamoja na vitanda "alisema Magige

Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais  ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi



Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha  Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuhaidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa  huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25  uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

No comments: