Saturday, June 17, 2017

NISHUSHE IDD MOSI... WASANII WATAKAOLIAMSHA DUDE, DAR LIVE

 Mashabiki wakiwa ndani ya Dar Live.


SIKU zikiwa zinahesabika kuelekea Usiku wa Nishushe Dar Live utakaofanyika Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar, wakali kibao watakaoliamsha dude siku hiyo wamefungukia makamuzi watakayotoa. 

Katika usiku huo, pazia la burudani litafunguliwa rasmi mapema kuanzia saa 8:00 asubuhi ambapo burudani ya watoto itatolewa chini ya kundi la sarakasi na kudensi la Wakali Dancers pamoja na Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania. Wakizungumza na Mikito Nusunusu kwa nyakati tofauti, wakali hao watakaoongozwa na R.O.M.A Mkatoliki walisema kuwa wataliamsha dude mwanzo mwisho sambamba na kutoa sapraizi kibao jukwaani.ROMA “Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa. Safari hii nisingependa ikupite hii. Nimepona na nipo fiti hivyo mje kwa wingi kushuhudia shoo yangu ya kwanza tangu mwaka huu uanze nikikinukisha kwa ngoma kali kuanzia Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao.”Darasa Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya.



[/caption] DARASA “Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya nikiwa na ngoma ya Taifa ya Muziki. Safari hii nakanyaga tena jukwaa hilo Idd Mosi nikiwa na ngoma nyingine ambayo nayo ni habari nyingine ya Hasara Roho. Sina maneno mengi; ‘Dunia iweke tuzo za wachukiaji, Bongo kuna watu wana vipaji, Utarusha madongo kwenye maji, Bora upige michongo utanipa midadi.’ Mr Blue akiwapagawisha mashabiki wake.[/caption] MR BLUE “Sikukuu hii ya Idd Mosi sehemu pekee ya kijanja ni Dar Live tu! Nitaliamsha dude na ngoma zangu zote kali kama Pesa, Mboga Saba, Baki Na Mimi na nyingine kibao. Muhimu mashabiki wajitokeze kumuona Byser mpya najua mnajua muziki wangu jukwaani upoje. Haina kukata pumzi hiyo!”STAMINA “Sina maneno mengi ila jukwaa linaongea. Battle za jukwaani kama kawa, mashabiki wajiandae kumsikia na kumuona Stamina akiwa na ngoma kibao mpya ikiwemo Love Me na siku hiyo ni mperampera mwanzo mwisho hadi kuchee.” [caption id="attachment_70948" align="alignnone" width="800"]Snura Akifanya yake ndani ya Dar Live na wacheza shoo wake.[/caption]SNURA “Nina zawadi kibao za kuwapa mashabiki wangu Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live. Mbali na kuwaimbia nitawaonesha live staili ya kucheza nyimbo zangu zote kuanzia Ushaharibu, Majanga, Chura, Najidabua, Shindu hadi wa sasa huu wa Nionee Wivu nilioimba na Yamoto Band.” BAMBO “Nitaliamsha kuanzia asubuhi mpaka mida ya jogoo akitoka bandani. Mkongwe niliyebaki katika uchekeshaji Bongo nitakuwepo kufanya yangu kwa watoto na wakubwa wote watakaofika Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live.” ZANZIBAR STARS Mmoja wa wanaounda Kundi la Zanzibar Stars, Sabaha Mchacho alisema; “Zanzibar Stars itazaliwa upyaaa Idd Mosi Dar Live. Wapenda Muziki wa Mwambao hii si ya kukosa kwani tumewaandalia vibao vipya kabisaa kutoka kwa wakali wengi wakiwemo Bi. Mwanahawa, Jokha Kassim, Mosi Suleiman na Zubeda Mlamali MTONYO JE? Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliweka wazi kuwa licha ya uwepo wa wakali wengi, kiingilio kwa siku hiyo upande wa shoo ya kibabe itakayoanza saa 8:00 usiku kitakuwa kiduchu yaani shilingi 7,000 huku watoto kikiwa shilingi 3,000 tu na bonasi ndani yake ya kuteleza bure, kubembea bure, kupanda ndege bure, kuogelea bure na vingine vingi bureee. (STORI: MIKITO NUSUNUSU, RISASI JUMAMOSI) 

No comments: