Saturday, June 17, 2017

"NEXT EINSTEIN" YAZINDUA WIKI YA SAYANSI AFRIKA TANZANIA

Mtaalamu wa masomo ya Sayansi, Fadhil Leonard akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza gari linalojiendesha bila ya kuwa na dereva wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sayansi Afrika Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam leo. 
Mtaalamu wa masomo ya Sayansi kutoka Shule ya Ilboru Arusha, Vedasto Biyaka akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza magari hayo.
Wanafunzi wakipata maelekezo ya kutengeneza magari hayo kutoka kwa mtaalamu wa masomo ya sayansi, Gibson Kawago kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
Mtaalamu wa masomo ya Sayansi kutoka Shule ya Ilboru Arusha, Vedasto Biyaka akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza magari hayo.
Wanafunzi wakiendelea kujifunza kutengeneza magari hayo.
Balozi wa NEF, Aneth David ambaye ni mwanataaluma wa sayansi na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akizungumza na wanahabari kuhusu kongamano hilo.
Wanafunzi wakielekezwa jambo kwenye hafla hiyo. 



Na Dotto Mwaibale

KONGAMANO la Next Einsten (NEF) ambalo ni mpango wa Taasisi ya kuendeleza Hisabati na Sayansi Afrika (AIMS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Robert Bosch Stiftung leo imetangaza uzinduzi wa wiki ya sayansi Afrika kupitia kongamano la NEF jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano hilo jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa NEF, Aneth David ambaye ni mwanataaluma wa sayansi na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kongamano hilo wanataaluma wa ndani, mabingwa wa sayansi na teknolojia wataongoza kwenye tukio hilo.

"Kongamano la Next Einsten la wiki ya sayansi Afrika ni wiki la kwanza la sayansi kuratibiwa ndani ya Afrika" alisema David.

Alisema lengo la msingi la kongamano hilo ni kuendeleza wanasayansi na wanateknolojia wa kesho kwa kuwahusisha watoto na vijana katika shughuli za kisayansi kama vile kujumuika pamoja na kushiriki maonesho.

"Shughuli zetu pia zitaonesha matokeo chanya ya sayansi kwa jamii nzima kwa kuwakutanisha wadau muhimu kutoka sekta zote na kuchochea uwekezaji katika tafiti na maendeleo pamoja na kujadiliana njia nzuri za kuwavutia na kuendeleza vijana hususan wasichana na wanawake katika nyanja ya sayansi" alisema Rais wa AIMS ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa NEF, Thierry Zomahoun.

Alisema wiki ya Sayansi Afrika inayofanyika hapa nchini itashuhudia vipindi vya kusisimua kama vile kuhusisha wanafunzi katika kujifunza kwa vitendo somo la kemia, Teknolojia na Uhandi kwa kutumia vifaa shirikishi vya sayansi ambapo pia wanafunzi watashiriki katika shughuli za vitendo na mashindano ya miradi ya sayansi na baadaye kufuatia na sherehe ya kutoa tuzo kwa washindi.

Kongamano hilo linafanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Seminari ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam.

No comments: