Thursday, June 8, 2017

MWENGE WA UHURU WAACHA HAMASA KITUO CHA WATU WALIOADHIRIKA NA DAWA ZA KULEVYA SOBER HOUSE

Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour (aliesimama) akizungumza na katika kituo cha Sober House wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga (aliesimama) akizungumza wakati wa Mwenge wa Uhuru ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House , Al –Karim Bhanji (katikati)akizungumza jinsi wanavyoendesha kituo hicho wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwasili katika Kituo cha Sober House

Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya pamoja na Watendaji wa Kituo hicho.
Mkurugenzi wa kituo hicho,Al –Karim Bhanji (katikati) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru
Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwaaga viongozi na Watendaji wa Kituo hicho.
Mwenge wa Uhuru
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour amewaasa watendaji mbalimbali nchini kuwajali vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali pale inapotokea.

Kiongozi huyo ameyasema leo wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipopita katika mradi wa kituo cha watu walioadhirika na Dawa za Kulevya Sober House Kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani,

Amesema kuwa vijana ndio wamekuwa waathirika wakubwa katika matumizi ya dawa za kulevya ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Nae Mkurugenzi Kituo hicho, Al –Karim Bhanji amesema vijana walioadhirika na dawa za kulevya wanatakiwa kupewa upendo kuwaacha kunaweza kukasababisha kurudi katika matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema kuwa wanashauri ambao ndio wanawashauri juu madhara ya matumizi ya dawa hizo pamoja na njia za kuweza kuepukana nazo.

Bhanji amesema malengo ya kituo hicho ni kuwa na walimu ambao watakuwa wanawafundisha waathirika hao ili kurudi kuendesha biasghra kutokana na elimu itakayotolewa na kituo hicho.

Amesema kuwa kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia kituo kituo kitaanzisha darasa la komputa ambapo waathirika watajifunza na wengine wanaweza kuwa na ujuzi tofauti.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga amesema kuwa Mwenge umeweza kupita miradi mbalimbali ambapo Sober House ni mradi ambao umeokoa vijana wengi ambao walitumbukia kwenye matumizi ya dawa za Kulevya.

No comments: