Monday, June 5, 2017

MSIUZE hOVYO CHAKULA KABLA YA KUWA NA AKIBA YA KUTOSHA- RC TABORA

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuweka akiba ya chakula cha kutosha ili kuepuka njaa inayoweza kuwakabili kutokana na mavuno ya msimu huu kutokuwa mazingira kufuatia mvua kuchelewa kuanza na kuwahi kukatika.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yalifanyika katika Manispaa ya Tabora.

Alisema mvua za msimu huu zilikuwa kidogo na hivyo mavuno ya mazao kama vile mahindi , mpunga na maharagwe ni hayaridhishi hivyo ni vema wananchi wakahakikisha wanatenga chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi yao kabla ya kuanza kuuza.

Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mikoa mbalimbali wamekuwa wakipita katika maeneo mbalimbali ya vijiji na kuwarubuni wakulima wawauzie mahindi yao nao bila kuchukua tahadhari wanafanya wamekuwa wakiuza bila kuweka akiba ya kutosha jambo ambao sio jema.

Aliongeza kuwa watu aina hiyo ambao wanakimbilia kuuza mahindi yao bila kuweka aakiba ya kutosha kwa ajili ya familia zao ndio wamekuwa wakimbilia kwa viongozi wa Serikali wanaishiwa chakula.

Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa ameamua kuwatahadharisha mapema ili kila mkazi wa Tabora akatumia fursa hii ya upatikanaji wa vyakula vya kutosha katika masoko kuweka akiba kwa ajili ya familia zao badala ya kukaa ili kugonja msaada na wakati mwingine kulaumu Serikali bila sababu za msingi.

“Nawaombeni tunzeni chakula mlichokipata kwa ajili ya matumizi ya baadaye badala kukimbilia kuuza na kutengenezea pombe za kiinyeji…jambo hili ni hatari kwa kuwa unapokosa chakula unageuka mtumwa na wakati mwingine unaweza hata kudhalilishwa na mtu mwenye chakula” aliwatahadharisha wakazi wa Tabora

Aidha Bw. Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanasimamia zoezi la kufanya tathimini ya chakula kilichopo katika maeneo yao na kuhakikisha hakuna uuzaji wa holela holela wa mahindi ili kuchukua tahadhari ya kukabiliana na tishio upungufu wa chakula kwa wakazi wa Tabora.

Alisema kuwa mtu asiuze chakula kama hana akiba inayoweze kumfikisha mkulima katika mavuno ya msimu ujao.

Bw. Mwanri alisisitiza kuwa Wakuu hao wa Wilaya wahakikishe viongozi wote wa Serikali za Vijiji na Mitaa wanasimamia zoezi la kuhakikisha kuwa mtu anayeuza mahindi anayo akiba ya kutosha na sio vinginevyo ili kuepuka tabia ya watu kukimbilia kuuza mahindi hivi sasa wakiishiwa wanaanza kukimbilia kwa viongozi.

No comments: