Mratibu wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara yake ya tatu.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Abdalla Mohd akizungumza na washiriki wa resi za baskeli kabla ya kuanza rasmi zikiwa na lengo la kuimarisha huduma za afya Hospitali ya Kivunge na Makunduchi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
Washiriki wa Bike Ride 2017 wakijaanda na safari ya kilomita 300 itakayowachukua muda wa siku sita kuzunguka kisiwa cha Unguja.
Washiriki wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya viwanja vya Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua sita sita.
Picha na Makame Mshenga.
…………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Fedha hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.
Akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka Uingereza amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar wanashiriki.
Amesema fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi na zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na Makunduchi.
Amesema Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.
Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.Akizindua resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.
Amesema pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni sehemu ya kuwashawishi vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.
Dkt. Fadhil amesema wakati serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja Hospitali ya Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika kuanzisha majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.
No comments:
Post a Comment