Friday, June 23, 2017

MILIONI 110 ZATOLEWA KUSAIDIA HUDUMA YA MAJI KIKWAJUNI

 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez,akifunga bomba la maji katika moja ya maeneo ambayo Mradi wa Maji Kikwajuni ushakamilika. UNDP wameahidi kuchangia   kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akisadiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), kumtwisha mkazi wa jimbo hilo ndoo ya maji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maeneo ulikopitia Mradi wa Maji Kikwajuni. UNDP wameahidi kuchangia   kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.Kulia ni Katibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYI inayosimamia mradi huo, Abdallah Ahmed Suleiman.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza katika mkutano na wananchi wa eneo la Kikwajuni Mao, alipowatembelea baada ya kukagua maeneo unakopita Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 110 kupitia UNDP kukamilisha mradi huo.
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kikwajuni Mao, katika mkutano huo aliongozana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib.UNDP wameahidi kuchangia  kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha Mradi wa maji katika jimbo hilo.
Mkazi wa Jimbo la Kikwajuni, Mohamed Seif Said, akijiandaa kumvisha zawadi ya kofia Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kuzungumza na wananchi katika mkutano uliohusu Mradi wa Maji jimboni hapo ambapo UNDP waliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib.
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez(kulia) na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib, walipotembelea maeneo yatakayopita mabomba yakusamabaza maji kwa wakazi wa jimbo hilo.UNDP wameahidi kuchangia  kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha mradi huo. Picha na Abubakari Akida.

 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib,baada ya kumaliza kutembelea maeneo ya Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha mradi huo.

Na Abubakari Akida
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limechangia kiasi cha shilingi 110 milioni katika kuwezesha huduma za maji kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kupitia Mradi wa Maji Kikwajuni uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar,Dk. Mohamed Shein miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo baada ya kutembelea vituo na vyanzo vya mradi huo vya Migombani na Kilimani, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP, Alvaro Rodriguez alisema lengo lao ni kuona jamii zinapata huduma mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo na wao wanachangia kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika.
“Nimeridhishwa na maendeleo ya mradi unaotarajiwa kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 10,000 wa jimbo hili, UNDP inajitolea kiasi cha shilingi milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika na wananchi wapate huduma ya maji,” alisema mwakilishi huyo wa UNDP
Akizungumza kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Salama Abood Talib, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha inashirikisha wadau mbalimbali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa wananchi wa maeneo mbalimbali visiwani humo na amemshukuru mwakilishi wa UNDP kwa msaada waliotoa katika kumalizia mradi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni amesema mradi huo una awamu tatu huku awamu mbili zikiwa  zishakamilika na wapo katika awamu ya mwisho ya kukamilisha mradi huo na  amemshukuru mwakilishi huyo  kwa msaada huo ambao utasaidia kukamilika haraka ili wananchi wafaidike na huduma hiyo.
Akizunguma kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Ahmed Said Makame alisema jimbo la Kikwajuni limekua na changamoto ya huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo na anashukuru mradi huo utakapokamilika tatizo hilo litakua limekwisha.
Mradi wa Maji Kikwajuni unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 344,000,000 ambapo awamu ya kwanza na ya pili ikiwezeshwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mbunge wa Jimbo hilo, michango ya wananchi na Serikali ya Japan. Mradi huo utakapokamilika utanufaisha wakazi zaidi ya 10,000 wa jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar.

No comments: