Sunday, June 11, 2017

Mazishi ya Shekhe Malilo yafanyika mkoani Kigoma

 Waumin wa dini ya Kiislam wakisalia mwili wa Marehemu Sheikh Taufiq Malilo aliyekuwa Sheikh wa mkoa Kigoma kabla ya mwili huo kupelekwa makaburi ya Kazaroho kwa mazishi.
 Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa
 Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa


Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kigoma.

HATIMAYE aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma kwa zaidi ya miaka 30 Taufiq Malilo amezikwa huku sehemu kubwa ya wananchi wa mkoa Kigoma wakijitkeza kuhudhuria mazishi hayo.


Shekhe Malilo ambaye alifariki Ijumaa jioni ya wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari na moyo amezikwa juzi jioni katika makaburi ya Kazaroho Ujiji mjini Kigoma.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika majira ya saa 11 jioni yaliacha vilio na simanzi kwa mamia ya waislam waliohudhuria msiba huo wengi wakikumbana mafundisho ya dini ya kislam katka kuishi maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu.

Wakati Mwili wa Shekhe Malilo ukipelekwa kaburini kwa ajili ya safari yake ya mwisho hapa duniani ili baadhi ya barabara kufungwa kwa muda ikiwemo sehemu ya barabara ya Lumumba ili kupisha umati mkubwa wa watu kutumia barabara hiyo kwa muda wakati wa kuelekea makaburini.

Akisoma Wasifu wa marehemu Katibu wa BAKWATA wilaya ya Kigoma vijijini ,Sheikh Yassin Kabunguru alisema kuwa Alhaji Malilo alichaguliwa kuwa Sheikh wa mkoa Kigoma mwaka 1979 hadi mauti yalipomfika akiwa pia Ulamaa wa Taifa.

Sheikh Kabunguru alisema kuwa katika uhai wake Alhaji Malilo alifundisha dini na kutembelea misikiti zaidi ya 600 mkoani Kigoma akiweka kambi kwa ajili ya kufundisha dini na kufungua shule mbalimbali za kiislam mkoani Kigoma kwa juhudi kubwa ambayo aliifanya binafsi.

Akitoa mawaidha kabla ya kuelekea makaburi Sheikh Uwesu Mohamed alisema kuwa Alhaji Malilo aliishi katika misingi sita ya kiislam ambayo ilimfanya kuwa mcha Mungu,mnyenyekevu anayewapenda wengine,asiye na tamaa wala kujilimbikizia mali na kwamba Marehemu amekufa akiwa hana hata gari kutokana na sehemu kubwa ya kipato chake kutumia kuendeleza masuala ya dini.

No comments: