Kikao
cha Wanafamilia,Viongozi wa siasa na Viongozi wa Dini kikifanyika
nyumbani kwa marehemu Ndesamburo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi
yake.
Ndugu na Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo.
Baadhi ya Wabunge wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya wanandugu wa familia ya marehemu Ndesamburo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini
MAZISHI
ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa
wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82) yanataraji kufanyika kwa
siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2 wakitaraji kushiriki
katika mazishi hayo.
Shughuli
nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na sita katika uwanja wa
mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya Jumanne kwa ibada
itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa marehemu.
Hatua
ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili inatokana na uwepo wa
idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika maziko hayo ya
kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho ,shughuli
zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nne
,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo Amani Golugwa
amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kutoa
heshima za mwisho kwa Ndesamburo.
“Tumekua
na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na mashaurizano kuhusiana na
msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo wachungaji na
viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu Ndesamburo
yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.
Kutakuwa
na siku mbili za maombolezi,siku ya jumatatu mwezi huu tutakuwa na
state funeral (mazishi ya kitaifa) siku ambayo tutafanya kumbukizi ya
maisha yake na tunataraji kuwa na idadi kubwa sana ya watu”alisema
Golugwa.
Kwa
upande wake msemaji wa familia ambaye pia ni motto mkubwa wa marehemu
Ndesamburo,Sindato Ndesambur o alisema vikao mbalimbali vinaendelea kwa
ajili ya maandalzi ya mazishi na kwamba yanataraji kutanguliwa na
maandamano.
“Kama
unavyoonabado tunaendelea na vikao kwa sasa ,kuona namna gani tunaweza
kumuaga mzee wetu kwa heshima aliyojijengea kwa wakazi wa Moshi na taifa
kwa ujumla “alisema Sindato.
Alisema
wanatazamia kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo
taasisi mbalimbali za kidini,kiserikali pamoja na wafanyabiashara
watakao shiriki katika shughuli nzima ya mazishi .
Mapema
jana vilio na Simanzi vilitawala chumba cha kuhifadhia maiti katika
Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,wakati familia ya Marehemu Ndesamburo
ikiongozwa na mtoto wake wa Pili ,Lucy Owenya kushudia mwili wa
mpendwa wao ukiwa umehifadhiwa.
Wakati
kifo cha Mzee Ndesamburo kinatokea ,Lucy Owenya alikuwa akihudhuria
vikao vya Bunge la 11 ,vikao vya Bajeti ambapo alipata nafasi ya
kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha kabla ya kupokea taarifa
rasmi ya kifo cha Ndesamburo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri.
Majira
ya saa 11:45 familia ilifika katika hospitali ya rufaa ya KCMC huku
Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisimamia zoezi la kuomba
kuona mwili wa marehemu Mzee Ndesamburo ili kujiridhisha kama kweli baba
yao amelala mauti.
Michuzi
Blog ililifika KDC nyumbani kwa marehemu Ndesamburo na kushuhudia
maandalizi ya shughuli za maziko yakiendelea huku waombolezaji kutoka
maeneo mbalimbali ya pembe ya nchi wakifika kutoa pole kwa familia ya
marehemu.
Philemoni
Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa za mageuzi ambapo
katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa
Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la
madiwani wa manispaa ya Moshi.
Ndesamburo
maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi katka siasa na
biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake kwa meya
wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa
shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari
Wilayani Karatu mkoani Arusha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment