Wednesday, June 28, 2017

MAVUNDE AAHIDI KUZITATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya kutembelea maeneo ya katikati ya mji na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hasa wafanyabiashara ndogo ndogo.

Hatua hiyo ya Mavunde imetokana na Ofisi yake ya Mbunge kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kero zao na matatizo yao kila Alhamis(kero za Ardhi) na Ijumaa(Mambo ya kijamii).

Hata hivyo kwa siku ya leo kutokana na mapumziko ya Sikukuu ya Eid El Fitr, Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ameamua kutembea maeneo mbalimbali ya mjini katikati na kusikiliza kero za wananchi.

Maeneo aliyotembelea ni pamoja na eneo la ‘One way’ ambalo kuna wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo na barabara ya sita ambako ni maarufu kwa maduka ya simu katika kata ya Madukani.

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea wananchi hao, Mavunde ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya kero zinazowasibu wafanyabiashara hao.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyabiashara katika maduka ya simu barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye moja ya maduka ya simu eneo la barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Dodoma wakati alipotembelea maeneo mbalimbali ya mji.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akisalimiana na mmoja wa walinzi katika eneo la barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi katika maeneo aliyotembelea.

No comments: