Thursday, June 22, 2017

MASAUNI ASHIRIKISHA WADAU WA MAENDELEO KUENEZA HUDUMA YA MAJI KIKWAJUNI

 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa(UN)nchini,  Alvaro Rodriges (kushoto), alipotembelea Mradi wa Maji  Kikwajuni uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein miaka miwili iliyopita ikiwa ni juhudi za  Mbunge huyo kushirikisha wadau  katika kuhudumia na kutatua kero  mbalimbali za wananchi  wa jimbo hilo. Kulia ni Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas.na anayefuata ni Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman.
 Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman akimuonyesha Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini,  Alvaro Rodriguez (wakwanza kushoto),ramani ya mpango wa uboreshaji huduma ya maji katika jimbo la Kikwajuni.Mratibu huyo amefika jimboni hapo ikiwa ni juhudi za Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto) katika juhudi zake za kutatua changamoto za  huduma ya maji kwa wananchi.
 Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas, akitoa maelezo ya Mradi wa Maji Kikwajuni kwa Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea mradi huo uliopo katika jimbo la Kikwajuni,Zanzibar.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini,  Alvaro Rodrigues, akiangalia moja ya mabomba yanayotumika kusafirisha maji kwenda kwenye maeneo mbalimbali jimboni Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni hapo.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini, Alvaro Rodrigues, akizungumza na Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Mhandisi Mohamed Elyas, wakati akiwasili kutembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar(ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas(kulia) wakati wakiondoka baada ya kumuongoza Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini, Alvaro Rodriguez(kulia),  kutembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na wadau  katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni.
Picha na Abubakari Akida

No comments: