Friday, June 16, 2017

MANISPAA YA KINONDONI YATAKA BILIONI 4 ZILIZOPO KWENYE AKUNTI ZA KATA ZITUMIKE KWENYE MIRADI ILIYOKUSUDIWA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akizungumza wakatiwa kikao cha baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispa ahiyo Magomeni jijini Dar es Salaam, juni 15, 2017.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limeagiza kuhakikisha fedha zote zilizopo katika akaunti za kata zaidi ya Bilioni 4.9 zifanyiwe utaratibu wa manunuzi ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika kata hizo.

Maazimio hayo yamefikiwa katika baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo lililongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta .

Aidha baraza hilo pia limeridhia maombi ya kamati ya Fedha kwa kutaka kubuni vyanzo vipya vya fedha vitakavyosaidia Halmashauri hiyo kupata fedha zaidi licha ya baadhi ya vyanzo kuhamia serikali kuu. 

pia kikao hicho kilipitisha azimio la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo chake cha kizalendo cha kuhakikisha kuwa fedha za watanzania zilikuwa zinapotea kutokana na mchanga wa Madini uliokuwa ukisafirishwa nje kiholela unapangiwa utaratibu wa kunufaisha Serikali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli aakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo akichangaia katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kinondoni.
Afisa Utumishi wa Manispaa ya Kinondoni, Anna Mwakasyesye akijibu hoja za Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika kikao cha baraza.
Sehemu ya Madiwani walioshiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya KINONDONI.
Diwani wa Kata ya Kunduchi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Michael Urio akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo Magomeni jijini Dar es Salaam.
Diwani wa kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge akichangia mada katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo Magomeni jijini Dar es Salaam
Mchumi wa Manispaa ya Kinondoni, Eugene Haruna akijibu hoja za madiwani katika kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya KINONDONI
Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi (PMU) manispaa ya Kinondoni akijibu hoja za Madiwani wa Manispaa hiyo
Diwani wa kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni ,Thadey Massawe akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akijadili jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Viti Maalum CHADEMA, Caroline Kazinza akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.

No comments: