Thursday, June 8, 2017

IDARA YA SERA NA MIPANGO OFISI YA WAZIRI MKUU YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUIMARISHA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA MIFUMO YA TAHADHARI TANGA, KILIMANJARO NA ARUSHA


Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya kifaa cha kupima mvua kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea vituo hivyo vinavyotekelezwa na Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari uliopo Lushoto Mkoani Tanga Juni 6, 2017.
Mhasibu Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mazigo akiuliza swali kwa Mhandisi wa mitambo ya hali ya hewa Bw. Michael Minja wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 6, 2017 Lushoto Tanga.
Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya mtambo wa kisasa wa usomaji wa taarifa za hali ya hewa kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ulio chini ya Ofisi hiyo.
Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakinukuu maelezo ya Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Kilimanjaro, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Moshi Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Mto Pangani Bw. Vendelin Basso akiwasilisha utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kwa upande wa Bonde la Mto Pangani mkoani Kilimanjaro wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi huo uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 7, 2017.
Mratibu Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei akiwasilisha mada yake wakati wa mkutano wa kutathimini Utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa Bonde la Mto Pangani Mkoani Kilimanjaro Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Hydrojia kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw.Paul Damian akimuonesha Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Grace Moshi kifaa cha kusafirisha taarifa za kuongezeka au kupungua kwa maji mtoni (Intelligent Top Cap) wakati wa tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Juni 7, 2017 Mkoani Kilimanjaro.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia namna ya Kifaa cha kupima joto Ardhi (Themometer) ikiwa ni moja ya kifaa kilichofungwa katika Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari eneo la Lyamungu Wilayani Hai.
Msaidizi wa masuala ya Hali ya Hewa Bw. Mbaraka Shaghira (katikati) akieleza matumizi ya Kifaa cha kupima upepo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ili kuona Utekelezaji wake eneo la Kituo cha Tafiti cha Lyamungu Wilayani Hai.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la mto Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya kusoma kifaa cha kupima kina cha maji kwa Mchumi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Bivelyne Muchumbuzi kilichopo katika Mto Malala wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari chini ya Ofisi hiyo Juni 7, 2017

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments: