Thursday, June 1, 2017

HIFADHI YA TAIFA MIKUMI MKOANI MOROGORO NI MBUGA ZA WANYAMA AMBAYO HUJIVUNIA IDADI KUBWA YA WAGENI

Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro ni moja ya mbuga za wanyama ambazo kwa sasa hujivunia idadi kubwa ya wageni na wanyama makundi tofauti wakiwemo simba pia ni hifadhi ambayo hufikika kwa urahisi na kuwafanya wageni kuona wanyama kwa haraka. 

Hifadhi imeshirikiana na vijiji katika kuunda ujirani mwema kupitia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi ili kuhakikisha maafisa wa wanyamapori wanashirikiana na wanavijiji kulinda mipaka ya hifadhi ya taifa mikumi dhidi ya ujangili. 

Mbuga ya wanyama Mikumi hupokea wageni wa aina mabalimbali wakimiwemo wenyeji wakazi kwa vingilio tofauti ukilinganisha na watalii wandani ambapo vingilio vyao ni shilling 5700 kwa mtu mzima.
 Muongozaji wa hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa mkoani Morogoro Yuston Bonike akimuonyesha muandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Ashton Baraigwa mbegu ya mimea ambayo inaweza kuliwa na nyani kipindi cha ukosefu wa chakula na kumletea madhara na nyani huyo kugeuka kuwa kichaa.
Moja wa maporomoko ya maji kivutio ambacho kina patikana katika hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambacho hufikiwa kirahisi kwa njia ya miguu na hupatikana ndani ya msitu huo.
Moja ya mnyama anayepatikana katika hifadhi hiyo anayejulikana kwa jina maarufu “digidigi” akiwa ndani ya Msitu huo 
Hali halisi ya mazingira ya hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambapo ofisi zake hupatika hapo mbele
Mafundi wakiwa katika ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Lumango Wilayani Kilosa mkoani Morogoro mradi wa ujirani mwema unaotekelezwa na Hifadhi ya taifa mikumi kwa asilimia 70 huku wananchi wakichangia nguvu kazi kwa asilimia 30. Nia na madhumuni ya ushirikiano huo ni kulinda na kuhifadhi mipaka ya TANAPA pamoja na kutoa taarifa za ujangili.
Moja ya jengo la Zahanati ambalo limeanza kutumika katika Kijiji cha Ihombo kata ya Mikumi mkoani Morogoro ambayo hupokea wagonjwa wasiopungua 300 kwa mwezi mradi ambao ulitekelezwa na Hifadhi ya taifa Mikumi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema na ulinzi wa mipaka ya hifadhi hiyo.
Tembo nao ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi ya taifa Mikumi mkoani Morogoro ambao mara nyigi hupenda kutembea kwa makundi wakati wa kujitafutia malisho.
Kikundi cha utunzaji wa mazingira kinachotokana na mradi wa utalii wa kitamaduni wakiwa wameshikilia vikapu ambavyo vimetengenezwa na mifuniko ya chupa za maji ambayo wamekuwa wakiyaokota. Wa pili kutoka kulia ni katibu wa kikundi hicho Bw. Christandus Mdoe.
Wageni wa kitalii katika hifadhi ya taifa mikumi mkoani Morogoro wakijadiliana kitu nje ya ofisi ya mapokezi huku wakifurahia mazingira ya eneo hilo la wanyama wakionyesha jinsi walivyo na amani katika eneo hilo.
Silas Bakari fundi ujenzi wa nyumba za kitamaduni akionyesha matumizi ya vyumba katika maeneo ambayo yamejengwa na chupa ambazo huokotwa kandokando ya hifadhi ya taifa mikumi na maeneo mengine, jinsi ambavyo chupa hizo zitakavyoboreshwa na kuifanya nyumba kuwa kivutio ch a utalii wa kitamaduni kwa wageni. 

No comments: