Tuesday, June 13, 2017

Halotel yashusha Neema kwa wateja wake


Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua kampeni mpya ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo sambamba na kuzindua utaratibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea wateja wa Mtandao huo katika maeneo yote nchi nzima mjini na vijijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika soko la Makumbusho lililoko Kinondoni Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mr Nguyen Van Son, amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma za kampuni hiyo, wamepata mapokezi mazuri kutoka kwa watanzania ambao hadi sasa zaidi ya wateja milioni tatu na laki tano, tayari wamejiunga na mtandao huo na wanafurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu.

“Tunafarijika sana kwa namna ambavyo Watanzania wameendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa jamii hii, ni faraja kubwa kwetu kwamba katika kipindi hiki kifupi tumepata mafanikio makubwa na bado tunaendelea kupata wateja wanaojiunga na mtandao wetu siku hadi siku,” Jambo hili linatufanya tusilale tufikilie ni namna gani tunapaswa kuendelea kukizi mahitaji yao.

“Kuzinduliwa kwa kampeni hii itakuwa ni sehemu ya sisi kusogea karibu na wateja wetu, kuwahudumia pamoja na kuwasikiliza ni nini wanahitaji kutoka kwetu,” Tunaamini kabisa kwamba kuwa karibu na wateja wetu tutajenga mtandao bora kabisa utakao kuwa na huduma zinazolenga maisha halisi ya Watanzania.

Aidha Naibu Mkurugenzi huyo alitaarifu kuwa, Kampuni hiyo imeanza utaratibu wa kuwa na vifurushi Maalumu kulingana na maeneo na mahitaji ya wateja husika, Huku akitolea mfano wa kuwa na vifurushi maalumu kwa wateja wa Mtandao huo wa Zanzibar ambao wameanzishiwa kifurushi maalumu cha ZANZIBAR YETU, ambacho kwa watumiaji wa Halotel wataweza kuongea bure siku za mwisho wa wiki kwa shilingi 1000 pamoja na vifurushi vingine, Kwa wateja wapya wa mikoa ya Mbeya, Manyara, Pwani, Arusha, Kilimanjaro na Mara, Mkoa huo wanaweza kupata dakika 60 za kupiga simu bure ndani ya mtandao kila wanapoweka muda wa maongezi kwa siku 30 baada ya kusajili . 
 
Pamoja na Ofa ya Kiboko yao ambayo inapatika katika baadhi ya minara ya 3G ya mtandao huo.Naibu Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa, licha ya kuboresha na kutoa huduma zinazowalenga Watanzania, kampuni hiyo pia imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha Mawasiliano na ubora wa Mtandao huo ambapo hivi karibuni mtandao huo ulitangaza uwekezaji wa zaidi ya bilioni 200 kwa ajiri ya kuboresha ubora wa sauti na kasi ya intaneti, huku wakitarajia kuwekeza zaidi katika mwaka ujao wa fedha. 

Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Salim Selemani, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao. Pamoja nae katika picha ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Frank Mwakyoma na waendesha pikipiki wa kituo cha makumbusho.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Simon Mkumbo, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son, akitoa maelekezo namna ya kupata huduma za mtandao huo kwa baadhi wa wafanyabiashara wa nguo katika stendi ya Makumbusho mara baada ya kujiunga na mtandao huo, Kampuni hiyo imezindua huduma ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na mtandao huo pamoja na wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja wa mtandao huo.
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, kwa pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, wakitoa maelezo juu ya huduma za mtandao huo kwa wafanya biashara wa Matunda wa soko la Makumbuso, Wakati wa uzinduzi wa huduma ya” Switch to Halotel” yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Pamoja na wafanya kazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja. Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Tawi la Dar es Salaam Vu Huy Thiem.
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, kwa pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, wakitoa maelezo juu ya huduma za mtandao huo kwa wafanya biashara wa Matunda wa soko la Makumbuso, Wakati wa uzinduzi wa huduma ya” Switch to Halotel” yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Pamoja na wafanya kazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja. Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Tawi la Dar es Salaam Vu Huy Thiem.
 

No comments: