Thursday, June 8, 2017

DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege ameupongeza mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS na kueleza kuwa mfumo huo ni suluhusisho la hati zenye mashaka katika halmashauri mbalimbali nchini.

Mfumo wa FFARS unatekelezwa katika mikoa 13 kwenye halmashauri 93 kwa ushirikiano wa serikali na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) pamoja na Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS) unaofadhiliwa na watu wa Uswizi (Swiss Tropical and Public Health Institute). 

Akifungua mafunzo kuhusu mfumo huo kwa maafisa elimu kata na Waganga Wafawidhi katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala,yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama,Berege alisema mfumo wa FFARS ni mwarobaini wa tatizo la halmashauri kupewa hati zenye mashaka. 

Alisema mfumo huo utawezesha takwimu nyingi za halmashauri za wilaya kukusanywa kwa usahihi zaidi kutoka vituo vya kutolea huduma ambavyo vitakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo huo. 

“Takwimu ni tatizo la kitaifa,hivyo mfumo huu utasaidia kuondoa tatizo hili kwa kuongeza uwazi na umakini katika masuala ya uhasibu na utoaji taarifa za fedha”,alieleza Berege. “Halmashauri zimekuwa zikipata hati zenye mashaka kwa sababu uwekaji takwimu haupo vizuri,FFARS ni tiba ya hati zenye mashaka,pamoja na kuendelea kutumia njia za vitabu/makaratasi,ni vyema halmashauri zikawa tayari kutumia njia za ki- elektroniki katika utunzaji takwimu”,aliongeza Berege. 

Aidha alilishukuru Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kufadhili mradi huo na kuwataka watanzania kuutumia vizuri ili kuleta maendeleo katika halmashauri. 

Naye Mshauri wa Kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno alisema mafunzo ya FFARS kwa Maafisa elimu kata na Waganga Wafawidhi katika vituo vya afya yanatolewa na wahasibu wa halmashauri za wilaya waliopatiwa mafunzo hivi karibuni na maafisa kutoka PS3, HPSS na maafisa kutoka TAMISEMI ili nao wawafundishe watoa huduma wengine katika vituo vya kutolea huduma. 

“PS3,HPSS,TAMISEMI na wadau wengine tumeamua kutoa mafunzo kuhusu mfumo wa FFARS ambao utaanza kutekelezwa Julai 1,2017 ili kuwawezesha watumishi katika vituo vya sekta ya afya na elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo huu katika shule,zahanati,vituo vya afya na hospitali za wilaya”,alisema Otieno. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege akifungua kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya kutoka halmashauri hiyo leo Alhamis June 8,2017 katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akifungua mafunzo hayo.Kushoto ni Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno,kulia ni Mratibu wa PS3 Halmashauri ya Msalala,Elikana Zabron 
Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno akielezea malengo ya mafunzo ya mfumo wa FFARS 
Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno akizungumza ambapo alisema mwongozo wa FFARS upo katika mfumo wa kielektroniki na mfumo wa zamani ulioboreshwa wa kujaza katika vitabu kulingana na miundombinu iliyopo katika vituo vya kutolea huduma nchini Tanzania 
Mratibu wa PS3 Halmashauri ya Msalala,Elikana Zabron akizungumza ukumbini 
Mratibu wa HPSS halmashauri ya Msalala,Happiness Josephat akiwa ukumbini wakati wa mafunzo kuhusu FFARS 
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini 
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini 
Mhasibu wa Afya wa Halmashauri ya Msalala, Peter Mathew Swai akiwasilisha mada kuhusu FFARS 
Washiriki wakifuatilia mada 
Mafunzo yanaendelea 
Mshiriki akisikiliza mada na kuandika dondoo muhimu 
Mafunzo yanaendelea 
Washiriki wa mafunzo hayo wakifanya kazi za vikundi kuhusu namna ya kuandaa taarifa mbalimbali za miamala ya fedha 
Kazi za vikundi zikiendelea 
Washiriki wakiandika kazi ya kikundi 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka PS3, HPSS na washiriki wa mafunzo ya FFARS 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka PS3, HPSS na maafisa elimu kata kutoka halmashauri ya Msalala 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka PS3, HPSS,wakufunzi na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka halmashauri ya Msalala. 


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments: