Imeelezwa
kuwa sababu kubwa inayochangia watoto kuendelea kunyanyaswa na
kufanyiwa vitendo vya kikatili katika maeneo ya kanda ya ziwa ni jamii
kukosa elimu kuhusu haki za watoto pamoja na kukosekana kwa ushirikiano
pale kesi zinazopelekwa katika vyombo vya sheria.
Hayo
yamesemwa leo June 16,2017 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika
katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.
Matiro
alisema tatizo kubwa linalotokea wakati wa kutetea haki za watoto
wanapofanyiwa ukatili ni kukosekana kwa ushirikiano wa jamii na wazazi
pale kesi inapofika katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani hivyo
kusababisha kesi nyingi kufutika matokeo yake watoto wanaendelea
kunyanyasika.
“Naomba
tuweke mkazo zaidi katika elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto,jamii
ikibadilika tunaweza kumaliza tatizo la unyanyasaji wa watoto,wazazi
wakielimika watajitokeza katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi kwa
vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wao”,alieleza Matiro.
“Haki
za watoto zinadidimizwaa sana kanda ya ziwa hasa mkoani Shinyanga
kutokana na jamii kukosa elimu na kung’ang’ania mila na desturi
zinazomgandamiza mtoto hususani mtoto wa kike hivyo mashirika na
serikali tushirikiane kubadilisha fikra za jamii,wananchi wajue haki za
watoto na wazilinde”,aliongeza Matiro.
“Bado
kuna mambo yanawanyima haki watoto,watoto
wanabakwa,wanafukuzwa,wanalawitiwa na wengine hawapelekwi shule,yote
haya yanatokea kwa sababu watu hawana udhubutu wa kutoa ushahidi kwenye
vyombo vya sheria”,alieleza.
Katika
hatua nyingine aliwataka watoto kutambua haki zao na wawe
wanashirikishwa katika mambo yanayowahusu badala ya wazazi pekee
kujiamlia.
“Tunaposema
haki ya mtoto tunataka kwanza watoto wazijue haki zao,haki ya
kuthaminiwa,kupata elimu,malezi,kutambulika lakini pia
kushirikishwa,yapo mambo yanafanyika katika jamii zetu yanafanywa
kinyume na haki za watoto,jamii yetu inatakiwa kutambua na kuziheshimu
haki za watoto”,alisema Matiro.
“Ni
jukumu letu kumlinda mtoto,kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria na
serikali lakini pia kwa kuwa watoto ni taifa la kesho,tunapaswa
kuwafundisha stadi za kazi,kuwafundisha haki zao”,alisema Matiro.
MSIKILIZE HAPO CHINI MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
ANGALIA PICHA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa
maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya
Shycom Mjini Shinyanga.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo ambapo aliwataka watoto kusoma kwa bidii kwani elimu ni
mkombozi wa maisha yao
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali
zilizotengenezwa na watoto waliopo katika kituo cha huduma ya watoto
Shirika la Compassion katika kanisa la KKKT Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia masweta na nguo mbalimbali zilizotengenezwa na watoto hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia kazi za watoto hao
Hata mikate wanatengeneza.......
Mtoa huduma katika kituo cha huduma ya mtoto Compassion katika kanisa la KKKT Clara Charo,akisoma risala
Mwinjilisti Elisha Shayo akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kanisa la KKKT mjini Shinyanga
Watoto wakicheza wakati wa maadhimisho ya Mtoto wa Afrika June 16,2017
Watoto wakicheza
Meneja wa Benki ya CRDB Shinyanga,Said Pamui akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Kiongozi wa shirika la Compassion akizungumza
Zawadi ya jezi kwa watoto walioshiriki michezo wakati wa maadhimisho hayo
Mtoto akipokea zawadi ya saa
Maofisa wa Benki ya CRDB wakifungua akaunti kwa ajili ya mtoto Picha zote na Moses Kiamani - Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment