Na Fredy Mgunda, Mufindi.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi amefanikiwa kutatua tatizo la vitanda katika shule ya sekondari Isalavanu iliyopo Kata ya Isalavanavu kwa kutoa vitanda 35 ikiwa lengo la kuendelea kuboresha na kuinua elimu ya shule hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitanda hivyo alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na ziara yake akiyofanya wiki kadhaa zilizopita wakati alipozitembelea shule mbalimbali za jimbo la Mafinga Mjini kujua changamoto na kuanza kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
"Niligombea ubunge wa jimbo la Mafinga kwa lengo la kuleta maendeleo ndio maana Leo nipo hapa katika shule ya sekondari ya Isalavanu kuanza kuinua elimu ya shule hii kwa kuboresha miundombinu ya shule na baadae nitatu changamoto nyingine"alisema Chumi
Chumi aliwataka wanafunzi wa shule ya Isalavanu kusoma kwa bidii ili kuleta matokeo chanya katika jimbo la Mafinga Mjini kwa lengo la kumuongezea kasi ya kutafuta wafadhili wa kusaidia kuleta maendeleo katika jimbo la Mafinga.
" Kwa kweli najitahidi kutafuta wafadhili wa kusaidia kutatua changamoto za jimbo la Mafinga Mjini lakini wananchi wangu na ninyi wanafunzi mnatakiwa kunipa matokeo chanya na kufanya maendeleo yenu ya mtu moja moja na vikundi pia natamani siku moja kila sekta niwakute watu kutoka jimbo la mafinga Mjini" alisema Chumi
Aidha Chumi aliwaomba wanafunzi na waalimu kufanya jitihada kuhakikisha wanapata matokeo chanya ili kuitambulisha shule na jimbo la Mafinga Mjini kwa lengo la kuwafanya wananchi na viongozi wa serikali kuangalia shule hiyo kwa jicho la tatu.
"Mkifanya vizuri kwa kufaulu mitihani ya taifa mtasaidia kuitangaza shule hii na kunifanya Mimi iwe rahisi kutafuta wafadhili kwa kuwa mmefanya vizuri kwenye matokeo ndio maana naomba sana na kusisitiza kuwa naomba mfanye vizuri kwenye matokeo tu kila kitu kita kaa vizuri "alisema Chumi
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga aliiomba serikali kuingalia shule hiyo ili kuifanya kuwa moja kati ya shule bora hapa nchini kwa kuboresha miunombinu ya shule ili wanafunzi kusoma bila woga wala hofu pamoja waalimu kufundisha bila kuwa na woga wowote.
"Jamani mimi naomba kuwa muwazi kwa ukweli mbunge wetu Cosato Chumi anafanya kazi sana kwa kulitetea jimbo hilo hasa ukiangazia jinsi gani anazungumzia sana maendeleo ya wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa kwa ujumla" alisema Makoga
"Makoga aliwataka wananchi na wanafunzi kudhamini mchango wa mbunge huyo kwa mchango wake katika kuleta matokeo chanya ya jimbo na mkoa wa Iringa kwa ujumla hivyo anapaswa kupewa heshima kwa kazi anayofanya katika maendeleo ya yanayoonekana" alisema makoga
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo walimshukuru mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi kwa kutimiza ahadi yake ya kuwatatulia changamoto ya vitanda katika shule yao.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi akimkabidhi vitanda 35 Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga ndg Charles Makoga kwa ajili ya kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi wa shule ya Isalavanu iliyopo katika Wilaya ya Mufindi
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa sambamba n wanafunzi wa shule ya sekondari y Isalavanu pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga
No comments:
Post a Comment