Na Bashir Nkoromo
Hatimaye
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi na Mbunge
wa Kuteulia na Rais Alhaj Abdallah Bulembo, amemaliza ziara yake ya
Kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya Wilaya 47 za
mikoa hiyo.
Katika
ziara hiyo ambayo alianza May 26, 2017, aliihitimisha jana, Juni 10,
2017 katika mkoa wa Geita, ziara ikiwa imechukua zaidi ya wiki mbili,
ambapo mkoa wa kwanza kufanya ziara hizo uliuwa Dar es Salam na badaye
kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na
Geita ambao ndio mkoa aliomalizia.
Alhaj
Bulembo katika ziara hiyo ambayo haikuhusu Jumuia yake ya Wazazi
Tanzania, bali ya Kichama zaidi ilikuwa mahsusi kwa kuagizwa na Bosi
wake, Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, kwa lengo la kutoa shukrani
kwa wana CCM kufuatia kura nyingi walizompa hadi kukipatia Chama Cha
Mapinduzi kura nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015.
Hata
hivyo Bulembo anasema, Shukrani hizo, ni za awali kwa kuwa Mwenyekiti
Mwenyewe Rais Dk. John Magufuli atafanya ziara rasmi kutoa shukrani.
Katika
ziara hiyo, Alhaj Bulembo pia pamoja na mambo mengine ya kuhimiza
ujenzi na uimarishaji Chama na Jumuia zake, alikuwa na ajenda za
kufafanua kuhusu mabadiliko yaliyowaacha nje badhi ya waliokuwa Mabalozi
na pia kufafanua kwa kina umuhimu wa Mabalozi wapya waliopatikana sasa
na wale waliobaki kutokana na mabadiliko hayo ndani ya Chama.
Alhaj
Bulembo kwenye vikao vya ndani kwenye ziara hiyo alipata fursa za
kuwapiga msasa, kwa kuwapa darasa zito Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
katika Wilaya husika, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia zote za Chama,
Mabalozi na Watendaji wote wa serikali.
Mara
kadhaa alisisitiza umuhimu wa madiwani kuwa karibu na viongozi wa Chama
hasa mabalozi, ikiwa ni pamoja na kuwatambua kwa karibu hadi kwa majina
na kujenga mahusiano ya kawaida kwa lengo la kukuza ukaribu baina yao
na viongozi hao, siyo tu wa kichama bali hadi wa kifamilia.
Katika
hali ambayo haikuwa ikitarajiwa, katika wilaya karibu zote alizofika,
ilionekana dhahiri kwamba madiwani karibu wote walikuwa hawana mahusiano
ya kawaida na mabalozi, hali hii ilijidhihirisha pale Alhaj Bulembo
alipokuwa akiwasimamisha madiwani na kumuuliza kila mmoja alivyoshiriki
kwenye uchaguzi wa mabalozi, idadi ya mashina na majina ya mabalozi
katika kata zao.
Madiwani
wengi walijikuta wengine hawajui hata idadiya mashina katika kata zao,
na pia walishindwa kutaja idadi ya mabalozi kwenye eneo lao, na kutaja
majina ya mabalozi ndiyo ilikuwa kazi kubwa. Diwani alijikuta akitaja
balozi mmoja au wawili tu, kata nzima.
"Mnajua
lengo la mahusiano haya, ni kukirahisisha Chama kupata kura kwa urahisi
wakati wa uchaguzi, kwa sababu ninyi madiwani mkiwa mmeshajenga
mahusiano na Wenyeviti wenu wa mitaa na mabalozi hakutakuwa na kazi
ngumu ya kutafuta kura, na lazima mtambue kuwa Mabalozi ndiyo siri kubwa
ambayo hufanikisha ushindi wa CCM katika chaguzi", anasema Bulembo kwa
nyakati tofauti.
Mbali
na darasa alilokuwa akitoa kwenye vikao hivyo, katika ziara hiyo
amewesha CCM kujizolea wanachama wapya 376 ambao walikihama chama cha
Chadema na kujiunga na CCM, wakiwemo waliokuwa viongozi wa Chadema
katika vitongoji na Vijiji na aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya
Mbogwe mkoani Geita.
Baada
ya Makala hiyo fupi yafuatayo ni matukio katika picha katika ziara ya
mwisho wa ziara hiyo ambayo Bulembo aliifanya jana katika Wilaya za
Mbogwe na Geita mkoani Geita.
Mjumbe
wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisiriki kuapa wakati
wanachama wapya waliohamia CCM kutoka Chadema walipokuwa wakiapa na
kuungwa mkono na wanachama wote katika kiapo hicho
Wanachama wapya wa CCM wakiapa
Wanachama wa CCM wapya wakiapa huku wakiungwa mkono na wanachama wote waliokuwa ukumbini, kula kiapo hicho
Alhaj Bulembo akiwahoji baadhi ya madiwani kuhusu mahusiano yao ya karibu na mabalozi yalivyo
Alhaj
Abdallah Bulembo akiwa tayari kikabidhi kwa diwani fedha zilizochangwa
kwa ajili ya kumsaidia mlemavu mmoja aliyeomba msada wakati wa kikao
hicho
Alhaj Bulembo akikabidhiwa zawadi mwishoni mwa kikao hicho
Alhaj Bulembo akiagana na baadhi ya wanachama wakati akitoka ukumbini baada ya kikao hicho mjini Geita.
Alhaj Bulembo akiwa katika Kivuko cha mv Sabasaba tayari kwa safari ya kwenda Mwanza jioni.
Baadhi ya wandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wa Alhaj Bulembo wakiwa ndani ya Kivuko hicho
Alhaj Bulembo akiwa ameketi na kiongozi mmoja wa CCM katika kivuko hicho
Alhaj Bulembo akizungumza jambo na Doto wakiwa kwenye Kivuko hicho
Alhaj Bulembo akitoka kwenye Kivuko hicho mwishoni mwa safari. PICHA: BASHIR NKOROMO
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalah Bulembo akisaini kitabu cha wageni
baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa halmashauri
Kuu ya CCM Wilaya ya Mbogwemkoani Geita, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia
za CCM, Mbalozi na Watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo, jana, Juni
10, 2017.
Mjumbe
wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadi kutoka kwa
mmoja wa wanachama sita wa Chadema, waliotangaza kutahmia CCM wakati wa
kikao hicho.
Stephen Thobias akizungumza baada ya kutangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM wakati wa kikao hicho
Nyambina Chacha akizungumza baada ya kutangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa kikao hicho
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha kadi za Chadema
baada ya waliokuwa wanachama wa chama hicho kumkabidhi na kuhamia CCM
wakati wa kikao hicho. Waliosimama mbele ni wanachama hao baada ya
kukabidhiwa kadi za CCM
GEITA🔽
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCm Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa skavu baada ya
kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Geita mkoani Geita, jana.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akienda ukumbini baada ya
kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita mkoani Geita, jana
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini huku akishangiliwa kwa nderemo.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili meza kuu. Kushoto
ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzani, mkoa wa Geita, Mbunge wa
Bukombe Doto Biteko na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Wilaya ya
Geita Ahmed Mbaraka na Katibu wa CCM Wilaya ya Geita Muhoja mapande
Alhaj Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuketi ukumbini
Mwenyekiti
wa umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Geita AllyRajabu
kihamasisha wakati akisaliia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakiwa ukumbini
|
No comments:
Post a Comment