Thursday, June 8, 2017

BIMA YA JAMII KUTOKA VODACOM TANZANIA NA JUBILEE INSURANCE YAZINDULIWA MKOANI MWANZA

#BMGHabari Kampuni ya mawasiliano nchini ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Jubilee Insurance, kwa pamoja zimezindua huduma ya bima ya afya ili kuwawezesha wananchi kupata matibabu kwa gharama nafuu katika mkoa wa Mwanza. 
 Huduma hiyo ambayo pia inapatikana kote nchini, inajulikana kama "Jamii, Ngao ya Afya" ambapo itawawezesha wateja wa Vodacom waliojiunga na hudumaya M-Pesa kupata matibabu kote nchini katika hospitali na vituo vya afya vilivyoidhinishwa kutoa huduma hiyo. 
 Huduma ya matibabu ya Jamii huwawezesha watumiaji wa Vodacom kupata matibabu kwa gharama nafuu ambapo kwa mwanachama mmoja atalipa shilingi 7,000 kwa miezi mitatu, miezi sita atalipa shilingi 23,000 na kwa mwaka atalipa shilingi 44,000 ambapo atanufaika na huduma bora za matibabu. 
 Ni rahisi sana kujiunga na huduma ya bima ya afya ya "Jamii" kutoka Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jubilee Unsurance, wasiliana na mtoa huduma kwa wateja kwa kupiga nambari 0743 888 111 ama 0755 88 5515
Diwani wa Kata yaKirumba, Alex Ngusa, akizungumza jana kwa niaba ya Naibu Meya wa Jiji la Mwanza kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
Asma Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
Asma Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
 
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakimsikiliza kwa makini, Asma Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, wakati akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
 
Maureen Ndekana kutoka USAID akizungumzia huduma ya Jamii kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
Victoria Chale ambaye ni Meneja Mauzo na Usambazaji kutoka Vodacom Mwanza akiwahamasisha wakazi wa Jiji la Mwanza kujiunga na huduma ya afya ya Jamii-Ngao ya Afya ambapo wananchi wengi walihamasika kujiunga na huduma hiyo
  • Noel Mazoya ambayeni Meneja Masoko, huduma za kifedha kutoka Vodacom Tanzania, akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya afya ya Jamii-Ngao ya Afya kwenye viwanja wa Igoma Jijini Mwanza
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakishuhudia uzinduzi wa huduma ya Jamii-Ngao ya Afya katika viunga vya Igoma Jijini Mwanza jana
Shukurani za pekee ziwaendee Vodacom Tanzania, Jubilee Insurance, ADGE Point kwa ufadhili wa watu wa Marekani USAID kwa kuwafikia wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kunufaika na huduma ya Bima ya afya ya Jamii ambapo kwa mwezi mzima timu ya usajili wa huduma hiyo itazunguka maeneo mbalimbali ikiwemo minadani ili kuwasajili wananchi wote.
Pia ahsante kwa 102.5 Lake Fm Mwanza, kwa kujumuika kwenye kuhakikisha wananchi wote wa Mwanza wanaifahamu huduma hii ya "Jamii-Ngao ya Afya". Kwa msaada zaidi piga simu nambari 0743 888 111 ama 0755 88 55 15

No comments: