Tuesday, June 20, 2017

Biko yampatia Milioni 20 mshindi wa Handeni

WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ jana wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao Yahaya Ally Khamis, aliyeibuka na ushindi katika droo ya 15, iliyochezeshwa juzi Jumapili, huku akitokea wilayani Handeni, mkoani Tanga. Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani hapa katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni, mkoani Tanga, tayari kwa kuziingiza katika matumizi ya kumkwamua kiuchumi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mchezo wao ni rahisi kucheza na kushinda, tofauti na michezo mingine inayotumia akili nyingi pamoja na uzoefu wa kufuatilia mambo mengi ya kukuletea ushindi. Alisema Biko ili mtu ashinde ni kufanya muamala kwenye simu yake ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456, huku mchezaji akiwa haulizwi swali lolote kwenye simu yake.

“Biko hatuulizi mtu swali lolote na ndio maana zaidi ya mtu kufanya muamala ambao Sh 1,000 yake itampatia nafasi ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000 zinazolipwa kwenye simu mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi, huku nafasi nyingine ikiwa ni kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambayo Jumapili iliyopita tulimpata Khamis tuliyomkabidhi leo fedha zake.

“Tumefarijika kuja Handeni kumpatia fedha zake mshindi wetu, huku tukiwaasa Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kucheza Biko kwa sababu ni mchezo unaotoa ushindi mzuri na haraka, hivyo chezeni kwa wingi na mara nyingi zaidi ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi,” Alisema Heaven.

Naye Khamis alisema amekuwa mchezaji mzuri wa bahati nasibu ya Biko, jambo ambalo limemfurahisha kwa kiasi kikubwa baada ya kupata ushindi sambamba na kupelekewa fedha zake wilayani Handeni ambako ndiko shughuli zake za kilimo anakoendelea nako.

“Wakati napokea simu ya ushindi kutoka Biko hakika nilishusha pumzi na kumshukuru Mungu, maana pamoja na mambo mengine ya kimaisha ambayo nakusudia kuyafanya, lakini pia Sikukuu hii kwangu naisherehekea kwa shangwe ya aina yake baada ya kukabidhiwa fedha zangu,” Alisema.
 
Baada ya kukabidhiwa fedha hizo, mshindi mwingine wa Biko wa Sh Milioni 20 anatarajiwa kupatikana kesho Jumatano na Jumapili ijayo ikiwa ni mwendelezo wa kutoa mamilioni ya fedha kwa washindi wao wanaopatikana  kwa kucheza bahati nasibu ya Biko, huku mwezi pekee wakitoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa washindi ikiwa ni mwelekeo mzuri wa mchezo huo.

Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 Yahaya Ally Khamis, dakika chache kabla ya kuelekea katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni walipomkabidhi pia kiasi cha fedha taslimu Sh Milioni 20 kama mshindi wa droo ya 15 ya Biko iliyochezeshwa Jumapili iliyopita. Wengine ni majirani na wadau wa Khamis, wilayani Handeni wakishuhudia wakati anakabidhiwa hundi hiyo.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis kulia. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni mkoani Tanga jana. Kushoto ni afisa wa NMB, wilayani Handeni akishuhudia makabidhiano hayo.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yahaya Ally Khamis, akiwa katika uso wa  furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni, mkoani Tanga jana, baada ya kuibuka na ushindi katika droo.

No comments: