Baadhi yetu
huwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi,
bwege, nk). Sahihi ni “mtindio ubongo” –
kwa Kiingereza “Down Syndrome”....
Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu,
kigugumizi, mwili mfupi, utofauti wa tambo la kichwa,vidole vya mikono
na miguu,nk.
Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio
Ubongo “ (Down Syndrome) alikuwa mshindi
wa kimataifa wa upigaji picha.
Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro
akaeleza:
“Wametoka vijana wengi kwenye nchi zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena
wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa
familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama
walivyoweka huku, picha yake
imeshinda...”
Mwasisi wa kujitolea
wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony
Teri Pettite na wazazi wake Samwel,
Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa
Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo. Picha na Habari za Freddy Macha
Samwel Mwanyika na picha iliyonyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini kwake, Ijumaa 16, Juni 2017.
Balozi Migiro, na Afisa Utawala Ubalozi London wakiwa na Samwel Mwanyika na mwenzake mwenye “Mtindio Ubongo” (Down Syndrome), Penina Haika Petitte.
Picha ya pamoja. Toka kushoto, Mjomba wake Sam, Hassan Mshangama, Mama Sam, Sophie Mshangama, Mony Teri Pettite, Penina Haika Pettite, Balozi Migiro, Sam Mwanyika, Rosa Kitandula (Afisa Utawala Ubalozini), na Philip Mwanyika (Baba wa mshindi).
Balozi Migiro akiwasikiliza wageni na kuwapongeza.
Balozi Migiro akizungumza na Mony Teri Petitte mwasisi wa “Pearl of People with DownSyndrome” anayejitolea kuendesha Jumuiya ya Watanzania wenye Mtindio Ubongo .
Tuzo ya Stephen Thomas
Tuzo ya Stephen Thomas
No comments:
Post a Comment